WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,akizungumza wakati
akifungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,akisisitiza jambo wa washiriki wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga ,akizungumza wakati wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salama za Mkoa wake ka washiriki wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
Rais wa Chama Cha Wataalam wa Mipangomiji Tanzania, Dk.Juma Matindana,akizungumza wakati wa Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji Prof.John Lupala,akielezea lengo la Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
MSAJILI wa Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji, Lucas Mwaisaka,akitoa taarifa ya Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi Bi.Immakulata Senje,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,(hayupo pichani) kufungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula,akitoa tuzo kwa mshiriki mmoja aliyefanya vizuri mara baada ya kufungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji ulioanza leo Machi 29 hadi 30,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk.Angeline Mabula ,amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za mitaa kupima, kulinda na kusimamia maeneo yote ya umma na maeneo ya wazi ili kuondokana na mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo.
Agizo hilo amelitoa leo Machi 29,2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipango Miji.
Dk.Mabula amesema Wakurugenzi hao wanapaswa kulinda maeneo hayo ili kuondokana na mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo.
“Umejitokeza utaratibu mbaya na usiovumilika, wa kuvamia maeneo ya wazi, maeneo ya umma pamoja na maeneo hatarishi na kuyabadilisha kuwa ya matumizi mengine, hasa makazi, maeneo hatari kimazingira pamoja na maeneo ya wazi, yakiwemo maeneo maalum kwa matumizi ya baadaye yanapaswa kupimwa, kumilikishwa na kulindwa dhidi ya wavamizi,”amesema Dk.Mabula
Amesema kuwa ili tuwe na mijini nadhifu na iliyopangwa vyema katika nchi yetu hakuna budi kuanza kusimamia upangaji wa miji midogo na vitovu
vya vijiji.
“Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2022 inaonyesha kuwa miji inakuwa kwa asilimia 4.8 na taarifa tulizonazo tuna jumla ya miji midogo inayochipukia 4310 nchini ambayo isiposimamiwa ipasavyo itakuwa miji holela ya baadae,” Amesema
Na kuongeza”Kwa kutambua umuhimu wa miji hiyo na uwepo wa kasi ndogo ya upangaji wa vijiji nchini, Wizara imeandaa mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini ili kuwezesha jamii yetu kuanza kupanga maeneo yao kuanzia vijijini,” amesema waziri Mabula
Aidha ametoa maelekezo kwa Bodi ya Usajili wataalam wa Mipangomiji na wanataaluma wote kuweka mkazo Zaidi katika namna ya kuzuia miji yetu midogo na vijiji kuwa makazi holela yabaadae
kwa kusimamia na kuelimisha jamii matumizi ya mwongozo wa upangaji na
ujenzi wa nyumba bora vijijini.
Hata hivyo amesema Pia Serikali itaendelea na jukumu lake la kuimarisha mahusiano ya kitaasisi ili kuimarisha maendeleo ya miji pamoja na kupata fedha kwa ajili ya kupanga na kusimamia miji.
”Naelekeza kuwa gharama za kuweza kumudu kupanga, kupima na kumilikisha maeneo yote nchini ni kubwa,Ninaelekeza Mamlaka za Upangaji nchini kutenga fedha kutokana na mapato ya ndani ya kila mwaka, kwa ajili ya kazi ya kupanga,kupima, kumilikisha,kuendeleza na kusimamia miji katika maeneo yao.”amesisitiza Waziri Mabula
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Anthony Sanga,amesema kuwa sasa ni wakati wa kujikita kwenye TEHAMA ili kurahisisha wananchi kupata huduma kwa haraka na kuondokana na migogoro ya ardhi.
Awali, Msajili wa Bodi ya Usajili wa Watalaam wa Mipangomiji, Lucas Mwaisaka, amesema kuwa watalaam wa mipangomiji 508 wamesajiliwa huku kati yao 36 wamefutiwa usajili kwa kukiuka maadili ya taaluma hiyo.