*******************
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako na doria za nguvu na zenye tija katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na kupata mafanikio makubwa ikiwemo kukamata watuhumiwa 14 kati yao wanaume ni 11 na wanawake 03 wakiwemo watuhumiwa wa kusafirisha vipodozi vyenye viambata sumu na kukamata wahamiaji haramu.
WAWILI WATIWA MBARONI WAKISAFIRISHA SHEHENA YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU KWENYE TANKER LA MAFUTA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva wa Lori @ Tanker la Mafuta aitwaye FAHMI AHMED [33] Msomali, Mkazi wa Dar-es-Saalam Mtaa wa Kigambon Soweto akiendesha Gari yenye namba za usajili T. 900 DEV na tela namba T.800 DEL aina ya Axon Benzi mali ya Feet Logistic Ltd pamoja na kondakta wa gari hilo MOHAMED MAWAZO [26] Mkazi wa Dar-es-Salaam Mtaa wa Mabibo kwa tuhuma ya kusafirisha vipodozi vyenye viambata sumu aina mbalimbali boksi 1,052.
Watuhumiwa walikamatwa Machi 25, 2023 majira ya saa 03:30 asubuhi huko eneo la Kijiji cha Songwe, Kata ya Bonde la Songwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya vijijini baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kupata taarifa za siri na kuweka mtego uliofanikisha kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa wamepakia na kusafirisha shehena ya vipodozi vyenye viambata sumu boksi 1,052 kwenye vyumba vya kubebea mafuta aina ya Petrol/Diesel wakitokea nchini Kongo na kuingiza nchini.
Vipodozi walivyokamatwa ni:-
- Epiderm box 38,
- Coco pulp box 159,
- Citro light box 87,
- Carolight box 152,
- Prety white box 22,
- Coco pulp maji box 100,
- Gluta white box 59,
- Diproson box 41,
- Pawpaw box 91,
- Extra clair box 50,
- Clear therapy Ct + box 164
- Betason box 72 na
- Nacitro light box 87.
Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikisha mahakamani.
Sambamba na hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia raia wa Somalia 12 kati yao wanaume 09 na watoto jinsi ya kike 03 kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali.
Watuhumiwa walikamatwa Machi 27, 2023 katika misako inayoendelea mkoani Mbeya wakiwa katika Lodge iitwayo Rubi iliyopo wilayani Kyela wakijiandaa kwenda nchini Malawi.
Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
- IBRAHIM HUSEIN MUHAMED [42],
- ABDIKAFI ABDALLAH HASSAN [26],
- RAMADHAN MAKKA TAJU [26]
- MUHAMED MACHA NURIA [26],
- ABDIRAHAMAN MUHAMED ALLY [27],
- MUHAMED AHMED ALLY [20],
- FAUD MUHAMED JIMALE [19],
- ABDIRAHAMAN HAMDI SAMARI [20],
- HANAD AHMED MUHAMED [22],
- JAWHARIA IBRAHIM HUSEIN [08],
- SADIA IBRAHIM HUSEIN [15] na
- SALMA IBRAHIM HUSEIN [08]
Watuhumiwa waliingia nchini Tanzania kupitia njia zisizo rasmi bila kuwa na vibali vinavyowaruhusu kuingia nchini.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuachana na biashara haramu/magendo, usafirishaji na uingizaji wa bidhaa zilizopitwa marufuku nchini kwani zinasababisha madhara kiafya kwa watumiaji. Aidha tunawataka wageni [Raia wa kigeni] kufuata utaratibu na sheria zilizopo za kuingia nchini ili kuepuka hadha na usumbufu wa kukamatwa. Tuendelee kuwahakikisha wananchi kuwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lipo makini na imara katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao., halitasita kumkamata wala kumuonea muhari mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na uhalifu.