Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima Akizungumza wamachinga hao katika viwanja vya soko hilo Mkoani Tabora wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa wamachinga Zuberi Omary na aliyekaa kulia ni kaimu mkurungezi wa manispaa ya Tabora Dkt Neema Kapesa .
Viongozi mbalimbali wakiwa wakimzikiliza waziri Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima.
Na Lucas Raphael,Tabora
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima ,ameagizwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Dkt Peter Nyanja kufanyamaboresho katika soko la Wamachinga Complex lililopo eneo la stedi mpya ya mabasi mkoani Tabora..
Akizungumza na wamachinga hao katika viwanja vya soko hilo Mkoani Tabora akiwa katika ziara yake ya siku mbili ambayo aliweza kukutana na Makundi Mbalmbali ya jamii na kuwasikiliza kero walizonazo ili aweze kuzitatua.
Dkt Dorothy Gwajima aliwaambia viongozi hao kwamba Maboresho hayo yatafanyika kutokana na fedha za bajeti ya halmashuari ya manispaa ya Tabora.
Alisema kwamba kama halmashauri ya manispaa ya Tabora inataka kwenda sawa na wamachinga wawashirikiane kwa kila kinachoendelea katika bajeti ambayo imetengwa katika halmashauri yao.
Dkt Gwajima alisema kwamba viongozi mkoani hapa wanapaswa kukaa na wafanyabiashara hao ili kuzungumza nao na waweze kujua bajeti ni kiasi gani kwa mwaka ,hali hiyo itafanya soko hilo kuwa katika hali ya utulivu mkubwa na malalamiko yataondoka.
Aidha alisema kwamba pamoja na bajeti hiyo inayokwenda kutengeneza miundombinu kwa mkutasari shirikishi wa kutoka ofisi ya maendeleo ya jamii kwa sababu wao ndio watu wao.
Hata hivyo Dkt Gwajima aliwaagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batrida Buriani na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Louis Bura wafuatilie ili atakaporudi tena asikute malalamiko juu yao na viongozi watendewe haki.
“Naamini kuwa maboresho hayo yatakayokwenda kufanyika yataondoa mapungufu yaliyopo katika soko hilo la wamachinga Complex Mkoani Tabora”alisema Dkt Gwajima .
Hivyo waziri alisema kwamba mikoa yote ilipaiwa Ramani na Mpango wa maendeleo ya masoko na Michoro ili wamachinga washirikishwe na hati zao ipatikane na namba zijulikane.