***************
NJOMBE
Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe,imefunga ushahidi wa kesi No 2 ya mwaka 2022 ya madai ya fidia ya Milioni 100 dhidi ya kanisa KKKT Dayosisi ya kusini iliyofunguliwa na msimamizi wa mirathi wa marehemu Kaselida Mlowe baada ya kifo kilichotokana na ajali,
Mahakama imefunga ushahidi na Kisha kuweka bayana kuwa April 18 mwaka huu itatolewa hukumu ya kesi baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote ambapo katika upande wa mdai mahakama imepokea ushahidi kwa msimamizi wa mirathi Sigrada Mligo huku katika upande wa utetezi ambao ni Kanisa la KKKT Mahakama imewasikiliza mashahidi wawili ambao ni Rajab Kitwana (35) aliyekuwa dereva wa gari ya Kanisa pamoja na Petro Kilima (41)
Katika upande wa mashahidi wa utetezi wakati wakitoa ushahidi mbele ya mahakama wamekiri kwamba hukumu ya kesi ya kwanza ambayo ilikuwa Traffic Case ilikuwa sahihi baada ya dereva kukutwa na makosa pamoja gari la kanisa kukutwa likiwa na hitirafu ya breki pamoja na kutokuwa na bima lakini wameomba mahakama kutupilia mbali kesi hiyo ili wazungumze nje ya mahakama kwa kutoa rambirambi ya mil 2 kwa familia ya marehemu alikatishwa Maisha kwa ajali.
Kesi hii ya Madai ni matokeo ya humu ya kesi ya makosa ya usalama barabarani kesi No 6,2021 kutokana na ajali iliyotokea eneo la Kibena mlima wa Ichunilo mjini Njombe September 25,2020 ikihusisha gari aina ya Hiace yenye Namba za usajili T298 DNE na gari yenye Namba T210-AHU Mercedes Benz Track Mali ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini na kupelekea kifo cha Kaselida Mlowe.
Kesi hiyo imeendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe Lihad Chamshama huku upande wa madai ikiwakilishwa na mawakili watatu akiwemo Emmanuel Chengula,Frank Ngafumika na Gervas Semgabo huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Marco Kisakali.