Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Mwanza(kulia) Mbunge wa Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mary Masanja (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi Mwanamke mjasiriamali mwenye changamoto ya ulemavu wa macho Matabu Tito kutoka wilayani Ilemela mkoani hapa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Sixbert Jichabu (kulia) Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mary Masanja ( wa pili kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite (wa tatu kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi mjasiriamali Jane Maira wakati wa ugawaji wa mitungi ya gesi na majiko kwa wanawaka wajasiriamali Mkoa wa Mwanza.Tukio hilo limefanyika leo Machi 27,2023 mkoani Mwanza.
Meneja Masoko wa Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba (katikati) akitoa elimu ya usalama wa matumizi ya gesi kwa wanawake wajasiriamali wa Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza kabla ya kupatiwa Mitungi ya gesi pamoja na majiko yake
Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite akizungumza wakati wa ugawaji wa mitungi ya gesi na majiko yake kwa wanawake wajasiriamali mkoani Mwanza
Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakishuka kwenye ngazi baada ya kupata mitungi ya Oryx pamoja na majiko yake
Mmoja ya Wanawake wajasiriamali mkoani Mwanza akiwa makini kupata mafunzo ya matumizi sahihi ya majiko ya gesi ya Oryx
****************************
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania ltd (OGTL) kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Wizara ya Utalii na Maliasili Mary Masanja kwa pamoja wameandaa mpango nishati safi ya kupikia kwa kugawa mitungi ya gesi zaidi ya 700 na majiko yake kwa wanawake wajasiriamali mkoa wa Mwanza.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi na majiko hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite amesema Mwanza ni moja ya mikoa nchini Tanzania iliyokuwa na eneo kubwa la msitu ambalo eneo kubwa limeharibiwa na ukataji mkubwa wa miti inayotumika kwa kuni na mkaa.
“Wakazi wengi katika eneo hili hutegemea kuni kwa kupikia na kupasha joto, lakini lazima watembee umbali mrefu kuzichukua. Wanawake na Watoto ni miongoni mwa walioathirika zaidi. zaidi ya hayo, kukusanya kuni sio tu kazi ya kusumbua lakini pia inaweza kuwa hatari sana kutokana na hatari za porini.
Ameongeza kugawa mitungi ya Oryx kunakwenda sambamba na utoaji mafunzo ya elimu ya kuhusu matumizi salama ya mitungi ya gesi ya Oryx na kuwawezesha kuhama kutoka matumiziya kunina mkaa kwenda kwenye matumizi ya gesi za kupikia (LPG.) ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kielimu na sera yake ya Mazingira, Kijamii na Kiutawaa(ESG).
Aidha amesema Oryx Gas Tanzania Ltd, “OGTL”, imeamua kutoa mafunzo ya nishati safi ya gesi ya kupikia kwa makundi mbalimbali ya watu nchini Tanzania. Mafunzo hayo yanalenga kutoa uelewa kuhusu LPG,
matumizi yake salama na jinsi kupikia kwa kutumia gesi ya LPG ili kuboresha afya ya jamii sambamba na kulinda mazingira.
“Kampeni hii ya Oryx Gas ni huu ni mwendelezo wa juhudi zetu katika kuunga mkono ajenda ya Serikai ya kutumia nishati safi kwa kupikia Watanzania wote, ikilenga kuona zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanatumia nishati safi kupikia ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa mitungi na majiko hayo huku yeye akiahidi kutoa Sh.30000 kwa kila mjasiriamali aliyepewa mtungi huo ili utakapoisha ajaze gesi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mitungi ya Oryx ,Masanja amesema kumekuwepo na juhudi mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
“Mfadhili wetu ametupatia nishati safi ya kupikia ili tuachane na kuni na mkaa , tunafahamu mitungi hii imejaa gesi lakini itaisha, hivyo nitatoa sh.30,000 kwa kila mjasiriamali ili aweze kujaza gesi itakapokwisha ili aendelee na shughuli zake za utafutaji.
Aidha amesema anatoka Wizara ya Maliasili na Utalii, hivyo anafahamu Mwanza imekuwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira.
“Gunia la mkaa linauzwa Sh.80,000 lakini unamaliza ndani ya muda sana, jiko la gesi na mtungi wake ni Sh.55000 ambalo lina gesi ndani yake na unapokwisha unajaza kwa Sh.24000, hivyo gharama ziko chini ukilinganisha na mkaa lakini ni rafiki wa mazingira,”amesema.
Amesema kuendelea kutumia kuni na mkaa kumesababisha vyanzo vya maji kukauka, kukosa hewa safi na mvua zinazonyesha hazina mpangilio kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi.