Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi pikipiki mmoja ya maafisa ugani wa wilaya hiyo kwa ajili ya kwenda kuboresha sekta ya kilimo kwa wananchi wa kata yake.
Hizo ndio baadhi ya pikipiki zikizokabidhiwa kwa watendaji wa kata na maafisa ugani wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
JUMLA ya pikipiki 54 wakabidhiwa maafisa ugani wa wilaya ya Nachingwea kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo ili kukuza uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo 54, Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa lengo la pikipiki hizo ni kukuza uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa wakulima wote wa wilaya hiyo.
Moyo alisema kuwa serikali imetoa pikipiki hizo 54 hivyo kila afisa ugani anatakiwa kupanga ratiba ya kuwatembelea wakulima na kutoa elimu ya kilimo kwenye maeneo husika ili wananchi walime kilimo kilichokuwa na tija katika maisha yao.
Alisema kuwa hategemei kuona pikipiki hizo zinatumika kinyume na malengo yaliyokusudiwa na serikali ya awamu ya sita ya kukuza sekta ya kilimo.
Moyo alisema kuwa lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ni kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo 2030 kwa ajenda ya 10/30 hivyo mnatakiwa wote kutekeleza majukumu yenu kama ilivyo.
Alisema kuwa anachotaka kukiona kwenye wilaya ya Nachingwea kwa kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao muda wote na wananchi wakafurahie huduma ambazo maafisa ugani mtakiwa mnatoa kwa wakulima.
Moyo alisema kuwa watawapima maafisa ugani baada ya kuwapatia vitendea kazi kwa kuangalia namna gani umekuza uzalishaji wa mazao toka wamepewa vitendea kazi hivyo.
Aidha Moyo alisema kuwa amegawa pikipiki tisa (9) na kofia ngumu kumi na nane (18) kutoka TAMISEMI kwa ajili ya watendaji wa kata kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi katika maeneo yao.
Alimazia kwa kuwataka maafisa ugani kuzitunza pikipiki na maafisa watendaji hizo kama mboni ya jicho lao ili ziweze kutumika kwa tija ya kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali kwenye kila kata.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea…… aliwataka watendaji na maafisa ugani kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kuondoa migogoro baina watumishi hao na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani
Aliwaomba watendaji na maafisa ugani kuzitunza pikipiki hizo kwa kuwa ni mali ya serikali ili zitumike kwa muda mrefu kwenye maeneo husika na kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.