RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa MNEC Ndg.Khamis Mbeto Khamis kwa kufiwa na Dada yake Marehemu Salma Mbeto Khamis, alipowasili katika viwanja vya msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja, kwa ajili ya maziko na kushiriki dua ya kumuombea marehemu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Salma Mbeto Khamis, ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa sala ya kumuombea Marehemu iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Bw. Salum Dimani, walipokutana katika maziko ya Marehemu Salma Mbeto Khamis, yaliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 24-3-2023, Marehemu ni Ndugu wa Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar.Ndg. Khamis Mbeto Khamis.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar.Ndg. Khamis Mbeto Khamis, baada ya kumalizika kwa dua na Sala ya kumuombea Marehemu Salma Mbeto Khamis, iliyofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 24-3-2023.(Picha na Ikulu)