Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mama Janet Mbene akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (Hayupo kwenye picha) Makao Makuu, Jijini Dodoma, mara baada ya kumaliza mazungumzo na Menejimenti ya REA
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mama Janet Mbene akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inayoongozwa na Mhandisi Hassan Saidy (Hayupo kwenye picha) katika ofisi za Makao Makuu ya REA, Jijini Dodoma,
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mama Janet Mbene akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ofisi za Makao Makuu ya REA, Jijini Dodoma, leo alasiri, tarehe 24 Machi, 2023. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia, Mhandisi Advera Mwijage, Meneja wa Kitengo cha TEHAMA, Bwana Frank Mugogo na wa mwisho ni Bwana Suleiman Byarugaba, Meneja wa Usimamizi wa Rasilimali Fedha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mama Janet Mbene akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ofisi za Makao Makuu ya REA, Jijini Dodoma, leo alasiri, tarehe 24 Machi, 2023. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Masoko na Teknolojia, Mhandisi Advera Mwijage, mbela yake ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy na anayefuata ni Bwana Renatus Nkwabi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa REA.
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy akiwa pamoja na Bwana Renatus Nkwabi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani pamoja na Mkurugenzi wa Fedha, Bwana Daniel Mungure pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango Bwana Nicolaus Moshi mwengine ni Mhandisi Thomas Mmbaga, Meneja Udhibiti Viwango wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mama Janet Mbene wakati wa mazungumzo yake na Menejimenti ya REA, Jijini Dodoma,
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mama Janet Mbene, tarehe 24 Machi, 2023 ametembelea kwa mara ya kwanza, ofisi za Makao Makuu ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA); zilizopo katika Jengo la PSSSF Makole, Jijini Dodoma na kuzungumza na Menejimenti ambapo, amepongeza kwa ushirikiano alioupata katika kipindi cha miezi mmoja tangu alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Mama Janet Mbene amesema, ushirikiano alioupata kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu na timu ya Menejimenti ya REA, inamwongezea ari ya kuwatumikia Wananchi wa vijijini ili kuhakikisha kuwa wanapata huduma ya nishati kupitia REA na kuahidi kuendelea kushirikiana ili Serikali ifikie adhima ya kuwaletea maendeleo Wananchi kupitia Sekta ya Nishati.
“Nimeiona hali ya Viongozi wa REA na nimependa uwazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku; Ninaamini sote tukishirikiana, hakuna jambo litakalokuwa gumu”.
“Kwa muda wa mwezi mmoja, tangu nilipoteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, kuwa Mwenyekiti, nimepata nafasi ya kufanya ziara kwenye maeneo mawili; Kwa dhati kabisa, namejionea namna Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini wanavyojitoa kwenye kutekeleza majukumu yao ya kila siku.”
“Jambo hilo, limenifurahisha na Mimi kwa upande wangu ninawaahidi ushirikiano”. Alisema Mama Janet Mbene, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini.
Mama Janet Mbene aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) tarehe 1 Februari, 2023 baada ya mtangulizi wake, kumaliza muda wake ambapo, tarehe 11 Februari, 2023 alianza kazi rasmi kama Mwenyekiti katika kikao chake cha kwanza, kilichofanyika katika ukumbi wa JNICC, Jijini Dar es Salaam.