Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg Abdulrahman Kinana akihutubia katika Mashindano ya Saba ya Quran yaliyoandaliwa na Faraja Islamic Foundation yaliyofanyika leo Machi 25 jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Faraja Islamic Foundation Sheikh Hashim madenge akizungumza katika Mashindano ya Saba ya Quran
Meza Kuu na Waumini wa Dini ya Kiislam Wakifuatilia Mashindano ya Saba ya Quran yaliyoandaliwa na Faraja Islamic Foundation yaliyofanyika leo Machi 25 jijini Dar Es Salaam.
Upande walioketi Wanawake Waumini wa Dini ya Kiislam Wakifuatilia Mashindano ya Saba ya Quran yaliyoandaliwa na Faraja Islamic Foundation yaliyofanyika leo Machi 25 jijini Dar Es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg Abdulrahman Kinana akikabidhi Zawadi kwa Ndg. Johari Muhunzi Mshindi wa kwanza Upande wa Juzuu Tano Katika Mashindano ya Saba ya Quran yaliyoandaliwa na Faraja Islamic Foundation yaliyofanyika leo Machi 25 jijini Dar Es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg Abdulrahman Kinana akikabidhi Zawadi kwa Ndg. Abdulkarim Bakari Auzi Mshindi wa kwanza Upande wa Juzuu Kumi Katika Mashindano ya Saba ya Quran yaliyoandaliwa na Faraja Islamic Foundation yaliyofanyika leo Machi 25 jijini Dar Es Salaam. (Picha Zote na Fahadi Siraji)
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewataka Waislamu kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) hususan kuhusu uchamungu na tabia njema.
Kinana ameyasema hayo leo Machi 25, 2023 wakati wa hafla ya mashindano ya Kuraani tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Faraja Foundation ya jijini Dar es Salaam.
“”Tunaagizwa na Kuraani, pia tunaagizwa na Mtume wetu (Muhammad – S A.W) kuwa kila Mwislamu anapaswa kuzingatia mambo mawili lakwanza ‘takwa’ (uchamungu) na lapili ‘akhlaki’ tabia njema).
“Kwahiyo ukizingatia ‘takwa’ ukazingatia na maadili mema hakuna namna utapotoka, itakuwa hakuna haja hata ya sisi kuwa na wasiwasi kwamba maadili mabaya yanaweza yakatupitia,” amesema Kinana.
Aidha, aliwahamasisha Waislamu nchini kuwapeleka watoto wao madrasa wakajifunze imani na maadili ya dini yao na kumjua Mwenyezi Mungu.