Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhe. Atupele Mwakibete, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duniani inayoadhimishwa machi 23 kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ilikua ni ,mustakabali wa hali ya hewa,tabia ya nchi na maji kwa vizazi vyote ,katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jana, jijini Dodoma.
*****************************
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Atupele Mwakibete amewataka wadau wa kilimo, nishati, maji, mifugo, uvuvi na wananchi kwa ujumla kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa mara kwa mara na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili kuweza kupanga na kutekeleza shughuli za kiuchumi na kijamii.
Ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani na kusema changamoto za tabia za nchi zimebadili majira na vipindi vya hali ya hewa hali inayoepekelea mabadiliko ya mara kwa mara ambayo bila kupata taarifa sahihi za hali ya hewa changamoto zitaongeeka hasa kwa wadau wa kilimo.
“Serikali imeamua kuhakikisha Sekta ndogo ya Hali ya Hewa inaimarika na taarifa zinadizi kuboreshwa ndio maana imetenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha rada zinafikia saba lengo ni ni kuwezesha uhakika wa taarifa kuongezeka”. Amesema Naibu Waziri Mwakibete.
Naibu Waziri Mwakibete ametoa rai kwa TMA kuhakikisha wanabuni mbinu mbalimbali ambazo zitafanya ya taarifa zinazotolewa kuweza kuwafikia wadau wakiwemo wakubwa na wadogo ili kuwafanya kuzitumia kwa shughuli zao za maendeleo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a amesema miongoni mwa juhudi zinazoendelea kufanywa kwenye utoaji wa elimu kwa umma ni pamoja na kufanya semina na warsha za mara kwa mara kwa waandishi wa Habari nchini ili kuwezesha wadau kupata taarifa kwa wakati.
Mkurugenzi Chang’a ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye Miundombinu kwani kwa kuwezeshwa kuwa na rada saba kutapandisha uhakikisha usahihi wa taarifa za utabiri kufikia zaidi ya asilimia 85.
Siku ya hali ya hali Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 23 ambapo Tanzania ambapo inaungana na nchi nyingine wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani (WMD) kauli mbiu ya mwaka huu imejikita uhamamsishaji wa matumizi sahihi ya maji ili kupunguza changamoto za tabia nchi zinazochangia mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.