Vyuo vikuu na Sekta mbalimbali vimeaswa kujadili kwa upana wake namna ya kupata ufumbuzi ambayo itatengeneza miongonzo mizuri ya kuisaidia nchi na kutatua matatizo ya jamii.
Hayo yamesemwa mapema leo Jijini Dar es salaam, na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), anayeshugulikia Utafiti, Prof. Nerisoni Boniphase kwenye Kongamano la siku moja la Mashirikiano kati ya Vyuo na Sekta binafsi linalounganisha wana taaluma kutoka vyuo mbalimbali na viwanda vya uhandisi hapa nchini lililofadhiriwa na Royal academy ya nchini Uingereza.
Prof. Boniphase amesema kuwa Chuo kimeunda kamati kwa ajili ya kuishauri chuo ambayo inahusisha wadau kutoka katika viwanda, serikali na mashirika mbalimbali ili wanafunzi kutambua changamoto zilizopo kwenye jamii na Teknologia na jinsi viwanda vinavyofanya kazi ili yale wanayowafundisha yaendane na mahitaji ya Wananchi.
Aidha amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ambayo inasisitiza mabadiliko ya mitaala ya elimu ambayo itasaidia fahamu matatizo ya jamii na kuweza kutatua kutokana na elimu waliopata hivyo kuja na suluhisho la matatizo ya jamii.
Amesema kuwa kuna pengo kubwa linaonekana katika mitaala ya elimu ambapo haliendani na wanafunzi wanavyotoka kwenye vyuo kutokana na teknolojia iliyopo kwenye soko hakiendani na la viwanda hivyo mjadala huo utaleta ufumbuzi wa kufundishwa mapema wakiwa shuleni.
Amesisitiza kuwa katika kuunganisha sekta binafsi na vyuo vikuu inatakiwa kuwepo kwa mashirano ikiwemo kufanya tafiti kwa pamoja ili kuleta ubunifu wa kutatua matizo yaliyopo.
Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano hilo Prof. Bavo Nyichomba amesema kuwa malengo yake ni kuboresha zaidi ushirikiano kati ya viwanda na vyuo vikuu hususani vya uhandisi.
Amesema kuwa ushirikiano huo pia utaenda kuanzisha uatamizi ambapo mwanafunzi na watu wa viwanda kufanya kazi kwa pamoja ikiwemo kwenye masuala ya kiutafiti ambayo yatasaidia taifa.
Pia ushirikiano huo utawezesha walimu wale wadogo pia kwenda kwenye viwanda ambapo wataenda kujifunza zaidi na kushirikiana na wanafunzi waliopelekwa na vyuo kutatua matizo ya viwanda.