Mkurugenzi Mtendaji wa ATE – Bi. Suzanne Ndomba akizungumza wakati akizindua Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE – Bi. Suzanne Ndomba akizungumza na wadau mbalimbali mara baada ya kuzindua Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************
NA MWANDISHI WETU
JUMLA ya Wanawake 73 wamejiunga na kuanza Mafunzo ya Programu ya Mwanamke Kiongozi ya awamu ya 9 yaliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Chuo cha Hisami na Kudhaminiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika la Waajiri .
Akizungumza katika hafla uzinduzi wa Programu hiyo leo Machi 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE – Bi. Suzanne Ndomba amesema progrramu hiyo ilianza mwaka 2016 na kuzinduliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu na tokea kuanzishwa kwake wamekuwa kimeendelea kufanya programu hiyo.
“Mwaka 2016 ambapo programu hii imeanza, imekuwa ikiendelea kukua ambapo kwa week iliyopita tulifanya mkutano wa mwaka wa mwanamke kiongozi ambapo wahitimu wa programu hiyo wa awamu ya nane waliweza kuhitimu masomo yao wanawake 65”. Amesema Bi.Suzanne.
Kwa upande wake Mkurugenzi Rasilimali Watu- CRDB , Bw.Godfrey Rutasigwa amesema kwa ushirikiano ambao wameufanya ATE na programu ya mwanamke kiongozi inamanufaa makubwa na wanawake ambao wanashiriki kwenye programu hiyo wengi wao wameonekana kuongeza utendaji kazi wao na kupata nafasi za juu zaidi za uongozi.
“CRDB Bank inaamini katika nguvu ya wanawake na katika kufanya hivyo tumekua tukiwekeza kila mwaka kwenye kuendeleza wanawake ambao ni wafanyakazi wetu ili waweze kukua na kushika nyadhfa kubwa mbalimbali za kiuongozi”. Amesema Bw.Rutasigwa.
Aidha amewashauri washiriki wote ambao wametoka kweye Benki ya CRDB wachukulie uzito suala hilo, wajifunze kwa bidii na kuhakikisha wanaweza kufanya vipindi vyote na kazi zote ambazo wamepewa na kuyachukua mafunzo hayo kwenda kuyaweka kwenye vitendo ili kuweza kuonyesha yale manufaa biashara yao kwa wafanyakazi wengine lakini pia wateja wanaowahudumia.
Naye Makamu wa Rais GGM- Bw. Saimon Shayo alisema lengo la kuwaleta wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ni kuwajengea uwezo ili waweze kuchukua nafasi za uongozi.
“Kwa desturi Duniani kote wanawake ni wachache kwenye sekta ya madini lakini kwenye uongozi pia ni wachache hivyo tunafuraha ya kwamba katika wale walioshiriki miaka ya nyuma tayari wamepata nafasi ya uongozi kwenye kampuni”. Amesema Bw.Shayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE – Bi. Suzanne Ndomba akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Rasilimali Watu- CRDB , Bw.Godfrey Rutasigwa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais GGM- Bw. Saimon Shayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Awamu ya 9 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyofanyika leo Machi 23,2023 katika Hoteli ya Sea cliff Jijini Dar es Salaam