Mratibu wa Mfuko wa kusaidia maendeleo ya vikundi vya wakulima wa mazao pamoja na misitu FFF(FAO) wanaotekeleza mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia ya nchi na uboreshaji wa maisha, Geofrey Bakanga akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha.
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja
Mmoja wa wajasiriamali wa asali kuonyesha bidhaa zake katika maonyesho hayo yanayoendelea jijini Arusha .
Julieth Lazier ,Arusha.
Arusha.Wafugaji katika sekta ya nyuki wamehimizwa kuzalisha mazao ya tokanayo na nyuki kwa viwango vya hali ya juu kwa kuzingatia ufugaji usioharibu
mazingira.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa misitu na nyuki kutoka wizara ya maliasili na utalii ,Emma Nzunda wakati akizungumza katika jukwaa lililohusisha wadau wa mazao ya ufugaji nyuki mkoani Arusha,lililoandaliwa na mtandao wa vikundi vya wakulima na ufugaji mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA) .
Emma amesema wizara imeendelea kuisaidia wajasiariamali wa sekta ya ufugaji nyuki kuyafikia masoko yatakayowasaidia kuongeza kipato kwa wafugaji bila kuathiri mazingira .
Kwa upande wake Mratibu kutoka Mfuko wa kusaidia maendeleo ya vikundi vya wakulima wa mazao pamoja na misitu FFF(FAO) ,Geofrey Bakanga amesema kuwa mfuko huo ni watekelezaji wa mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na uboreshaji wa maisha .
Bakanga amesema kuwa, kupitia mradi huo unaofanyika kwa kanda unalenga kuwafikia wakulima kwenye ngazi za wilaya na kunufaika na kuzilinda rasilimali zilizopo katika maeneo husika.
Hata hivyo jukwaa hilo la wazalishaji na wachakataji wa bidhaa za mazao yatokanayo na nyuki wanakutana kwa lengo la kuona namna bora na tija katika uzalishaji kwa mfugaji mdogo kupata mnyororo wa thamani .
Kwa upande wa kikundi Cha Msamaria farmers Group ambacho kilianza mwaka 2012 kikiwa na wanachama 12 ambapo kwa sasa kina wanachama 35 wamesema kuwa ,
wao wanashughulika na kilimo cha vanila pamoja kilimo cha Mahindi na maharage ,zao la kahawa na pamoja na Alizeti ambapo kinawasaidia kwa ajili ya kujipatia mkopo ili kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake Diwani mstaafu wa kata ya Leguruki wilayani Arumeru mkoani Arusha Anderson Sikawa amesema kuwa, amekuja na mazao ya asali wa nyuki wadogo na wakubwa na mizinga yake kwa lengo la kutoa elimu zaidi namna ya ufugaji bora na wa kisasa na wenye tija zaidi.
Amesema kuwa, asali ni dawa nzuri sana kwa watoto na watu wote kwa ujumla kwani asali ni chakula kisichokuwa na kemikali yeyote hivyo kinafaa sana kwa matumizi.
Aidha aliomba serikali iendelee kuwawezesha kujipatia vifaa vya utendaji kazi ili waweze kurahisisha shuguli za ufugaji nyuki nchini kufuatia soko la asali kuwa kubwa duniani.