Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi Kundo Mathew,akizungumza wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UCSAF Prof.John Nkoma,akizungumza wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) jijini Dodoma
Mhadhiri wa Chuo Kikuu UDOM Dkt.Florence Rashidi,akizungumza wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) yaliyofanyika jijini Dodoma
Mwakilishi Kutoka Benki ya NMB Bi.Neema Mgombela,akizungumza wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) yaliyofanyika jijini Dodoma .
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Mapinduzi kutoka mkoa wa Mara Violeth Emmanuel akitoa neno kwa niaba ya wanafunzi walionufaika na mafunzo ya TEHEMA wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyofanyika jijini Dodoma yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew ,wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew ,akiwakabidhi zawadi ya laptop Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mafunzo ya TEHAMA wakati wa Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT)
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga Kilele cha Mafunzo na Mashindano ya Siku ya Kimataifa ya Wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Na Erick Mungele-DODOMA
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amewataka wanafunzi waliopata mafunzo ya TEHAMA watakaporudi katika Shule zao kwenda kuwa mabalozi wazuri pamoja na kuwafundisha wenzao ili kuleta chachu katika kusoma masomo ya Sayansi.
Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akifunga kilele cha mafunzo na Mashindano ya siku ya Kimataifa ya wasichana na TEHAMA yaliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma( UDOM), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ( MUST) pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT).
Mhe.Kundo amesema Jumla ya wasichana 246 kutoka mikoa yote Bara na Zanzibar walishiriki mashindano hayo huku 31 wameshinda ikiwa ni mmoja kwa kila mkoa na juzi na kukabidhi kompyuta mpakato kila mmoja.
“Wanafunzi 31 walioshiriki katika kutengeneza applications hizo wamepatiwa zawadi ya laptops kutoka UCSAF, kila mmoja amepatiwa ya kwake kwa lengo la kuwahamasisha kuendelea kujifunza zaidi masuala ya TEHAMA.”
Mhandisi Kundo ameupongeza uongozi wa UCSAF ,DIT, UDOM na MUST kwa kusimamia uendeshaji wa mafunzo hayo kwa umahiri, huku akiwataka wanafunzi hao kwenda kuwa mabalozi shuleni na kuwafundisha wengine.
“Kwa nyinyi mliopata mafunzo kwa muda huu nendeni mkawe mabalozi kwa wanafunzi wengine maana TEHAMA ina mambo mengi lakini kwa mbeleni inaweza kuwasaidia kuingiza kipato maana mlichokifanya hapa si kidogo ni kikubwa sana,”amesema Mhandisi Kundo
Hata hivyo Naibu Waziri ameagiza bunifu za mitandao zilizoanzishwa na wasichana hao ziendelezwe na kila Wizara ichukue sehemu yake ili kuwaunga mkono kwa walichoanzisha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya UCSAF Prof.John Nkoma, amesema mfuko huo umejidhatiti kusimama na wasichana ili kuwawezesha kuwa na ujuzi wa Tehama.
“Lengo la mashindano ni kuunga mkono siku ya wanawake na Tehama ambayo kilele chake huwa ni Alhamisi ya nne ya kila mwezi April.”
Awali Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba amesema mpango wa kuwawezesha wasichana katika Tehama ni sehemu ya mkakati wao ambao wataendelea nao wakati wote na jumla ya wasichana 246 kutoka mikoa 31 ya Tanzania Bara wameshiriki mafunzo hayo.
Amesema katika mafunzo hayo ambayo yalichukua siku 5, wasichana 56 walikuwa katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia mkoani Mbeya(MUSTI) 96 walikuwa kwenye Taasisi ya Teknolojia(DIT) na 95 walikuwa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM).
” Katika mafunzo hayo, walibaini kuwepo kwa vipaji vya hali ya juu kwa wasichana ambavyo vinahitaji kuendelezwa ili kupata hazina za siku za usoni.”amesema
Akitoa neno la shukrani kwa niaba Mwanafunzi wa Sekondari Mapinduzi Mkoa wa Mara Violeth Emmanel ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha mafunzo haya kwa wanafunzi maana imewasaidia kujua TEHAMA kwa kuwa walipoanza mafunzo walikuwa hawanauelewa juu ya TEHAMA.
”Tunaiomba Serikali kuwawezesha mashuleni kuwa na Kompyuta ili kujifunza zaidi masomo ya TEHAMA zaidi lakani pia mafunzo yawe endelevu kwa wanafunzi wote kwa wa kike na wa kiume maana itasaidi wanafunzi kuendelea kutamni na masomo ya TEHAMA.”amesema Violeth.