Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo, Dkt. Daniel Mushi,akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika leo Machi 21, 2023 Jijini Dodoma
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Vidah Malle,akitoa elimu kwa washiriki ya kuwajengea uwezo na kujadili fursa za mkopo huo, wakati wa kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika Machi 21, 2023 Jijini Dodom
Mtendaji Mkuu kutoka kampuni ya FROSTAN, Bw. Luc Battel ,akiwasilisha mada wakati wa kikao cha uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika leo Machi 21, 2023 Jijini Dodoma
Mratibu wa dawati la Sekta binafsi lililopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Deogratius Gambago,akizungumza wakati wa kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika leo Machi 21, 2023 Jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo, Dkt. Daniel Mushi (hayupo pichani), wakati akifungua kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika leo Machi 21, 2023 Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kufungua kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika leo Machi 21, 2023 Jijini Dodoma
SERIKALI kupitia Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB) inatarajia kutoa mkopo wa Sh1.3 trilioni kusaidia wanawake kuboresha biashara na uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani katika sekta za mifugo na uvuvi.
Hayo yamesema na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na uvuvi Dkt. Daniel Mushi,wakati wa kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika leo Machi 21, 2023 Jijini Dodoma
Dkt.Mushi amesema kuwa dhumuni la fedha hiyo ni kuwezesha sekta binafsi kuwa kichocheo cha maendeleo.
“Kwa kuanzia walengwa mahsusi ni sekta binafsi hususan kwa biashara zinazoongozwa na wanawake au shughuli zinazoambatana na uchumi wa buluu ikiwemo kilimo cha mwani”alisema Dkt. Mushi.
Aidha Dkt. Mushi amesema sio tu kuwainua wanawake katika uwekezaji bali hata kuzalisha fursa za ajira kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya bahari na mifugo kwa ujumla na kupunguza suala la ukosefu wa ajira nchini.
“Wajasiriamali watumie fursa hii vizuri ili iwe kioo na baadae tuaminike ili fedha zijazo zipitie moja kwa moja kwenye sekta binafsi na fursa hii itakuja tena ikiwa tutakuwa waaminifu kwa kutumia vizuri mikopo hiyo”amesema Dkt. Mushi
Kwa upande wake Mchumi kutoka Wizara ya fedha na Mipango Vidah Malle amesema kuwa mkopo huo ni fursa pekee kwa sekta binafsi kukuza uaminifu kwa kutoa matokeo chanya ya fedha watakazozichukua.
“Sina uhakika kama fursa kama hii imewahi kupitia katika sekta binafsi mara nyingi hupitia Taasisi za Serikali kwa hiyo hii ni hatua nzuri na tumeoneshwa kuaminiwa hivyo tujitahidi tutakapopata fedha hizo basi tulete matokeo chanya”amesema Bi.Vidah.
Naye Kaimu Mkuu kitengo cha kilimo rejareja NMB, Wogofya Mfalamagole amesema kuwa benki yao imejipanga kutoa mikopo hiyo kwa wawekezaji wote kwenye sekta binafsi kwa mujibu wa taratibu walizopangiwa na Serikali kwa riba isiyozidi asilimia 10.
Awali Mwekezaji na Katibu wa Chama cha usindikaji wa maziwa Tanzania (TAMPA) bI.Rose Lyimo,amesema kuwa katika jamii kuna wanawake wengi wanaofanya shughuli za uwekezaji na hawana mitaji ya kutosha kupanua biashara hivyo mitaji hiyo itasaidia kuwainua wanawake na kuonyesha uwezo wao
Mkopo huo ambao unatajwa kuwalenga zaidi wanawake utakwenda moja kwa moja kwa sekta binafsi kupitia Benki za NMB, CRDB na KCB