Mkuu wa mkoa wa Tabora,Balozi Dkt Batilda Burian akipewa maelezo ya miradi ya maji na Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini wilayani Nzega mhandisi Gaston Nturo katika kijiji cha Isalalo kata ya Bukene wingine katika picha ni kushoto ni mkuu wawilaya ya nzega Naitapwaki Tukay kushoto kwa mkuu wa mkoani ni Mhandisi wa Ruwasa mkoa huo Hatari Kapufi na mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dkt Hamnisi Kingwangala
Mbunge Wa jimbo la Bukene Selamani Zedi Akimtwisha maji mama huyo katika kijiji cha Isalalo kata ya Bukene pembeni ni mbunge wa jimbo la nzega vijijini Dkt Hamisi Kingwangala aliyavaa suti ni Diwani wa kata ya Uduka ,Majonas Mshingo .
Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini wilayani Nzega mhandisi Gaston Nturo akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian juu ya miradi ya maji inayotekelezwa katika wilaya hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian akiwana mikono mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika kata ya Busondo wengine ni Diwani wa kata ya Busondo aliyesimama kushoto ni Affua Semwenda na mbunge wa jimbo la nzega .
Na Lucas Raphael,Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora,Dkt Batilda Burian,wamewapongeza wakala la maji na usafi wa mazingizra vijijini (Ruwasa) wilaya ya Nzega kwa usambazaji na upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kutoka asilimia 51 hadi kufikia asilimia 76 .
Kauli hiyo ilitolewa jana alipokuwa akizinduzi wa miradi mbalimbali ya maji katika kata za Bukene,Isalalo na Busondo,wilayani Nzega,mkoani Tabora.
Balozi Dkt Batilda Burian,alisema kwamba Ruwasa imeongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji maeneo ya vijijini ndani wa wilaya hiyo .
“Ruwasa inatekeleza miradi yenye ubora na kuongeza idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi kutoka asilimia 51.3 juni 2019 hadi asilimia 76.5 Desemba mwaka 2022” alisema Balozi Dkt Batilda .
Awali Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini wilayani humo mhandisi Gaston Nturo alimweleza mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt Batilda Burian, kwamba hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kiwilaya hadi kufikia mwezi Dedemba 2022 ilifikia asilimia 76.5 ikiwa ni sawa na uzalishaji wa maji lita milioni 15 .3 tu kwa siku .
Mhandisi Nturo alisema kwamba Ruwasa wilaya ya Nzega kuanzia mwaka 2019 imejenga miradi ya bomba 51 na kukarabati miradi ya maji ya bomba 52,kuchimba visima virefu 36 kwa gharama ya shilingi bilioni 18.3.
Alisema kwamba Miradi iliyofunguliwa jana ipo katika kata za Bukene,Isalalo na Busondo,wilayani Nzega,pamoja na mingine na kusisitiza kwamba Ruwasa itahakikisha huduma ya maji inapatikana muda wote.