Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam juu ya ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ya kutoa kiasi cha shilingi Milioni Mia tano endapo timu hiyo ikifanikiwa kutinga katika fainali za AFCON 2023, kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Khamis Mwinjuma na kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Saidi Yakub.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam juu ya ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ya kutoa kiasi cha shilingi Milioni Mia tano endapo timu hiyo ikifanikiwa kutinga katika fainali za AFCON 2023.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Khamis Mwinjuma (kulia) ambaye pia ni kiongozi wa msafara wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kikao na waandishi hao juu ya ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ya kutoa kiasi cha shilingi Milioni Mia tano endapo timu hiyo ikifanikiwa kutinga katika fainali za AFCON 2023, katikati ni Waziri wa wizara hiyo Balozi Dkt. Pindi Chana na kushoto Mkuu wa wizara hiyo Saidi Yakub.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akitoa ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ya kutoa kiasi cha shilingi Milioni Mia tano endapo timu hiyo ikifanikiwa kutinga katika fainali za AFCON 2023.
Picha na Eliphace Marwa – WUSM – Dar es Salaam