Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi ambae pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Biashara (ZNBC) Mhandisi Zena A. Said akitoa taarifa ya utekelezaji wa hoja zilizowasilishwa na Sekta Binafsi katika Mkutano wa tano wa Baraza la Taifa la Biashara la Zanzibar uliofanyika Tarehe 22 Januari,2023,wakati wa hafla ya jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Mfanya Biashara wa kuuza na kununua Fedha Hassan Ali Nahoda akitoa malalamiko kuhusiana na upatikanaji wa fedha za kigeni wakati wa majadiliano katika Jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais ,Fedha na Mipango Mhe.Sada Mkuya Salum akijibu hoja ya changamoto za upatikanaji wa fedha za kigeni wakati wa majadiliano katika jukwaa la kumi na mbili la Biashara la Zanzibar lililofanyika Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.