Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akitoa
taarifa ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ndani ya kipindi cha miaka
miwili tangu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aingie madarakani katika mkutano uliofanyika jana Machi 18, 2023 Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Na
Dotto Mwaibale, Singida
ILI kuunga mkono mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii
yaliyofikiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili ya
uongozi wake, viongozi wa dini mkoani hapa, wamewataka wakuu wa idara zote serikalini
kuweka mbele uadilifu na uaminifu katika matumizi ya fedha wana po tekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Wametoa nasaha hizo
jana Machi 18, 2023 wakati wa mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoahuu, Peter
Serukamba kubainisha mafanikio ya miaka Miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa
na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Tumesikia hapa fedha
zilizotolewa na Rais kwa ajili ya miradi mbalimbali yamaendeleo kwa mkoa wetu
(Singida), nitoe mwito kwa idara zote wawe waadilifu katika matumizi ya fedha zinazotolewa
na serikali kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Ni vizurizitumike
kulingana na taratibu, viongozi wawe waadilifu, wazipokee na kuzitumia katika unyenyekevu,
waige mfano wa Rais (Mama Samia) mwenyewe mnyenyekevu na mpole wawe na huruma na
upendo na watu.
“Viongozi msiishie
kusema mama anaupiga mwingi, taarifa ya leo ni hatua nzuri kwa taifa letu,”
alisema Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro.
Kwa upande wake
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kati, Dk.
SyprianHilinti, amewataka watendaji wanaomsaidia Rais mkoani hapa watekeleze miradi
ya maendeleo kwa haraka, ubora na mafanikio.
Alimpongeza Rais Samia
kwa uongozi wenye kasi yenye upendo na hekima na kwamba anamwombea aongoze kwa uadilifu
na amani.
Aidha, alimshukuru
mkuu wa mkoa Serukamba kwa kuwa kiongozi wa mfano mkoani hapa katika kutekeleza
majukumu mbalimbali ya kimaendeleo.
Askofu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Singida, Edward Mapunda,alisema maendeleo makubwa aliyoyafanya Rais Samia
katika kipindi cha miaka miwili ni ya Watanzania wote,hivyo ni vema wamwombee kwa
Mungu aliyetaka wakati huu awe rais wa Taifa hili ili azidi kutekeleza majukumu
aliyoitiwa na Mungu.
Awali Serukamba alisema
katika kipindi cha miaka miwili ya Utawala wa
Rais Samia miradi mingi ya kijamii na kiuchumi imetekelezwa mkoani hapa kutokana
na bajeti ya mkoa kuongezwa zaidi ya mara
dufu.
“Bajeti ya sekretarieti
ya mkoa imeongezeka kutoka sh. Milioni 180,187,060,500 mwaka 2020/2021
hadishilingi 239,808,971,000 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 33.09,”
alisemaSerukamba.
Aidha, alibainisha
kuwa Serikali Kuu imeidhinisha bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa mwaka 2022/2023
kwa ajili ya kuwalipa posho madiwani na watendaji kata na posho za mawasiliano
kwa watendaji wa vijiji kitendo ambacho hakikuwahi kufanyika katika awamu zote za
serikali zilizopita.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro Issa
akizungumzakatika mkutano huo kabla ya kumuombea dua Rais Dk.Samia Suluhu
Hassan kwa mafanikio makubwaambayo nchi imeyapata katika kipindi cha miaka
miwili tangu aingie madarakani.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dkt. Sprian Hilint akizungumza katika
mkutano huo.