Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt ,Batilda Buriani akikata utepe wa kuashiria kupokea shehena ya vifaa vya kwanza ya Mabomba ya kuweka Miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la kilimi wilayani nzega mkoani hapa ni kulia ni meneja wa shamba hili Jacob Chiwanga kulia na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge kushoto ni Das wa wilaya ya nzega Salaganda Lubugu na mkuruneze wa mji wa Nzega Shomari Mndolwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge wakiteta jambo na Mkurungezi wa uzalishaji Asa Dkt Jastin Ringo na aliyevaa tishet Nyekundu ni Meneja wa shamba la kilimi Jacob Chiwanga wakiwa wamesimama nyuma ya gari lililoleta mabomba kwa ajili ya miundombimu ya umwangilia .
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt ,Batilda Buriani pamoja na viongozi mbalimbali wa wakishuudia mkandarasi wa kampuni ya ProAgro Global Limited Mhandisi Nicolaus Maro akitandaza mabomba kwenye mtaro utakaopeleka maji kwenye shamba hilo.
mabomba wakiwa nje wa viwanja vya wakala wa mbegu bora za kilimo lililopo katika maeneo ya kilimi wilani Nzega Mkoani Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt ,Batilda Buriani kupokea shehena ya vifaa vya kwanza ya Mabomba ya kuweka Miundombinu ya Umwagiliaji katika Shamba la Wakala wa Mbegu za kilimo Kilimi Nzega Mkoani Tabora.
Akipokea vifaa hivyo vya Miundombinu ya Umwagiliaji katika Shamba la Kilimi Nzega alisema kwamba Serikali imedhamiria kuinua sekta ya kilimo hasa katika kuhakikisha upatikanaji wa Mbegu bora unakuwa wa uhakika.
Balozi Dkt Batilda alisema Serikali ya Mkoa wa Tabora itahakikisha inatoa ushirikiano wakutosha kwa shamba hilo hasa kuilinda miundombinu hiyo ya Umwagiliaji.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt Sophia Kashenge alisema kukamilika kwa miundombinu hiyo kutaongeza Uzalishaji wa Mbegu bora za kilimo tofauti na ilivyo sasa.
Alisema kukosena kwa miundombinu ya umwagiliaji katika Shamba la Kilimi kumesababisha hasara baada ya ekari 150 za mahindi kuosa maji na kusababisha kuwa ukame .
Dkt Kashenge alisema mashamba ya Wakala yanayowekewa miundombinu ya Umwagiliaji kupitia mradi huo ni pamoja na Shamba la Kilimi Hekta 400,Shamba la Msimba Hekta 200 na Shamba la Arusha Ngaramtoni Hekta 200.
Alisema matarajio ya Mkandarasi ifikapo mwezi Mei 2023 waanze majaribio ya kilimo cha umwagiliaji watakuwa wamekamilisha hatua ya kwanza ya mradi ya hekta 210 na wakati huo wakiendelea na hatua ya pili Kwa eneo lililobaki
Dkt.Kashenge aliipongeza Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuthubutu kutoa pesa na kuanza uwekezaji wa kilimo cha umwagiliaji.