Na John Walter-Manyara
Katika kuadhimisha wiki ya maji, iliyozinduliwa Machi 16, 2023 na waziri mkuu kasim majaliwa Jijini Dar es salaam, wakala wa usambazaji maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara wamewahimiza wananchi kufikisha huduma ya maji kwenye nyumba zao na kuacha kutegemea vituo vya umma.
Akizungumza na SMILE FM REDIO Afisa ustawi wa jamii RUWASA Amina Mwanja, amesema lengo la wiki ya maji ni kutoa elimu ya kutunza vyanzo vya maji na kuwaeleza wananchi shughuli mbalimbali ambazo ruwasa imefanya tangu kuanzishwa kwake.
Ameeleza kuwa Katika miaka miwili ya Rais Dr. Samia madarakani, serikali imewatengea fedha ambazo zimewasaidia kutekeleza miradi mbalilmbali maeneo ya vijijini na kuongeza upatikanaji wa maji ambapo kwa 2020/2021 RUWASA mkoa wa manyara ilitengewa sh bili 16.176 ambazo fedha hizo zilitekeleza miradi mbalimbali katika wilaya zote tano na kufanya upatikanaji wa huduma ya maji kufikia asilimia 5.07.
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 walitengewa bilioni 15 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali i na kuwahudumia wananchi 1,17,068 katika vijiji 37 kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Aidha mpaka kufikia mwaka 2025 wanatarajia kuwafikishia wananchi vijijini huduma ya maji kwa asilimia 85.
Kauli mbiu ya wiki ya maji kwa mwaka wa 2023 ni THAMANI YA MAJI KWA UHAI NA MAENDELEO.