Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt.Ahmed Makwani (katikati) akizungumza katika Maadhimishi ya Siku ya Utepe Mweupe Duniani, ambapo Kitaifa imefanyikia leo Machi 15,2023 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt.Ahmed Makwani akizungumza katika Maadhimishi ya Siku ya Utepe Mweupe Duniani, ambapo Kitaifa imefanyikia leo Machi 15,2023 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume akizungumza katika Maadhimishi ya Siku ya Utepe Mweupe Duniani, ambapo Kitaifa imefanyikia leo Machi 15,2023 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam.Mratibu wa Utepe Mweupe Bi.Rose Mlai akizungumza katika Maadhimishi ya Siku ya Utepe Mweupe Duniani, ambapo Kitaifa imefanyikia leo Machi 15,2023 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imesema licha yakuwa matokeo yanaonesha idadi ya vifo vya kina mama wajawazito kupungua hadi kifikia vifo 238 kwa kila vizazi laki moja bado eneo la kina mama na mtoto linakabiliwa na changamoto ikiwemo miundombonu ya majengo yenye staha kwa wakina mama wajawazito
Akizunguza Jana Machi 15,2023 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe Duniani, Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt.Ahmed Makwani amesema takwimu mpya za vifo vya mama na mtoto zinategemewa kutoka mwezi June “lakini kwa matokeo ya sasa kutokana na mwenendo wa mabadiliko yaliofanywa na Serikali, Tanzania imeonekana kufanya vyema kwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito kutoka vifo zaidi ya mia tano hadi vifo 238 kwa kila vizazi laki moja” .
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa mchango wa asasi ya Muungano waUtepe Mweupe hivyo basi wataendelea kutoa ushirikiano wa kutosha na kuhakikisha Vifo vya wakina mama wajawazito vinapungua ama kutokomezwa kabisa hapa nchini hasa kupitia jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume amesema Mkoa wa Dar es Salaam bado unakabiliwa na changamoto katika miundombinu ya afya ikiwemo majengo ya staha kwa wakina mama wakati wa kujifungua pamoja na magari ya wagonjwa.
“Katika Mkoa wetu wa Dar es Salaam, kwenye suala la magari ya kubebea wagonjwa bado ni changamoto kwani mpaka sasa tuna magari 11 kati ya 36 yanayohitajika kwenye Mkoa huu”. Amesema Dkt.Mfaume.
Nae Mratibu wa Utepe Mweupe Bi.Rose Mlai amesema katika Maadhimisho ya Mwaka huu ujumbe mkubwa ni uwepo wa huduma staha kwa wakina mama wajawazito huku ikiwa ni hali tofauti kwa baadhi ya hospitali ikiwemo hospitali ya Temeke ambayo ina shida ya jengo la kutolea huduma za wajawazito kwa staha pamoja na miundombinu itakayo wasaidia walemavu.
Siku ya utepe mweupe huadhimishwa kila ifikapo Machi 15 ambapo mwaka huu imeadhimishwa katika hospitali ya Temeke ikiwa ni kwa niaba ya mkoa wa Dar es Salaam huku hospitali hiyo ikikabiliwa na changamoto ya eneo finyu la wana mama wajawazito hali inayopelekea kina mama hao kulala watatu watatu katika kitanda kimoja.