Wabunge na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya uumma (pic) wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati hiyo hayupo pichani jana leo mkoani Tabora .
Mkurungezi wa mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira TUWASA Mayunga Kashilimu aliyevaa suti ya bluu akimuongoza mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (pic)Jerry Slaa kutazama miundombinu ya maji katika kjuji cha itumba kuona Tanki kubwa la kuhifdhia maji kutoka ziwa victoria lenye uwezo wa kuchukua lita milioni 9
Mkurungezi wa mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Tabora TUWASA Mayunga Kashilimu aliyevaa suti ya bluu akimuongoza mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (pic)Jerry Slaa na wajumbe wa kamati hiyo akitoa maelezo juu ya tanki la maji la kazehill lenye uwezo wa kuchukua maji lta milioni 5
******************
Na Lucas Raphael Tabora
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji imeiagiza bodi ya Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Tabora,Tuwasa,kuhakikisha wanaweka mpango madhubiti wa kuongeza mapato ya Mamlaka na kupunguza upotevu wa maji hadi asilimia 20 kutoka asilimia 27 ya sasa
Wakitoa maazimio ya kamati kupitia mwenyekiti wake,Jerry Silaa leo alisema lazima upotevu wa maji udhibitiwe na hivyo Tuwasa ifikie asilimia 20 ambayo ndio inaruhusiwa kimataifa.
Kamati pia imeiagiza Bodi ya Tuwasa,Kuongeza mkakati wa kukusanya mapato yatokanayo na matumizi ya maji ili iendelee kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Sanjali na maagizo hayo pia imeiagiza kuwa na utaratibu wa kuonyesha namna mradi ulivyoshiriki kutengeneza ajira kwa wananchi.
Mwenyekiti wa bodi ya Tuwasa,Dick Mlimuka,alisema wamepokea maagizo ya kamati na kwamba watayafanyia kazi na kuyatekeleza.
“Tunaishukuru kamati kwa maagizo yake ambayo tumeyapokea na tutayatekeleza.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa Tuwasa,Mayunga Kashilimu Taasisi za Serikali hazilipi kwa wakati 154milioni kwa mwezi ambazo zinachelewa kulipwa kama Majeshi na Polisi huku wananchi wanalipa kwa wakati tofauti na Taasisi za Serikali.
Wanauza 800milioni na kukusanya 700milioni lakini wanaangalia vipaumbele katika matumizi.
Gharama za matumizi ya maji zinakidhi uendeshajinwa mradi na maji yakifika Urambo,Sikonge na Kaliua malengo yatakuwa yamefikiwa kwa asilimia 100.
Juhudi zao wanataka kuongeza wateja zaidi ili gharama zishuke baada ya kukusanya zaidi.