***************************
*Ni mafanikio ya ya Miaka Miwili ya Rais Dk.Samia Hasan Suluhu
Na Mwandishi Wetu
Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita, Idadi ya makundi maalum iliongezeka kutoka 102 hadi 260 sawa na ongezeko la asilimia 154. Ambapo makundi ya wanawake ni 113, Wazee 15, Vijana 125 na watu wenye ulemavu ni Saba (7).
Kwa Mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma Bw. Eliakim Maswi alibainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wa mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan PPRA imekuwa ikihamasisha makundi maalumu kuchangamikia fursa zinazotolewa na sheria ya ununuzi.
Bw. Maswi alieleza Serikali iliamua kutoa fursa kwa makundi maalumu ambayo ni wanawake, vijana,wazee na watu wenye ulemavu kushiriki katika zabuni za umma kwa lengo la kumuinua mwananchi wa chini kiuchumi.
Amebainisha kuwa utekelezaji wa sheria hiyo kwa miaka miwili umezaa matunda makubwa na kupelekea baadhi ya makundi maalumu kunufaika na mpango huu wa Serikali
Bw. Maswi ameeleza kuwa PPRA imeweza kutoa elimu na kuhamasisha umma kutumia fursa hiyo iliyowekwa na Serikali.
“Tumepata mafanikio makubwa katika ongezeko la makundi hayo hasa zaidi kundi la wanawake” Alisema.
Mamlaka iliendesha kampeni maalumu ya uhamasishaji kwa wananchi kujiunga katika vikundi na kujiirodhesha PPRA.
Kampeni hiyo ilifanyika katika mikoa nane ya Tanzania Bara ambapo mwitikio wake ulikuwa ni mkubwa kwa jamii.
Mamlaka imejipanga kuendelea na kampeni mbalimbali za uhamasishaji ili kuhakikisha inatimiza lengo la Serikali ya awamu ya sita ya kuinua kipato cha wananchi wa chini.
Mamlaka imeendelea kusimamia kwa ukaribu mipango ya mwaka ya ununuzi ya mwaka (APP) ili kuhakikisha kila taasisi inatenga asilimia 30 ya zabuni zake kwa ajili ya makundi maalumu, kama inavyoelekezwa na sheria ya ununuzi.
“Nazikumbusha taasisi nunuzi kuendelea kutenga fedha hizo kwa ajili ya makundi hayo”. Alisema.
Maswi alieleza utaratibu wa makundi hayo kuingia katika ununuzi wa umma wanatakiwa kuwa wamesajiliwa katika Halmashauri au taasisi wezeshi yoyote iliyo na uwezo wa kusajili makundi hayo kama Ofisi ya Waziri Mkuu na Vyuo vya ufundi (VETA).
Amesema sharti la kuzingatia katika makundi hayo, uongozi wa kundi ni lazima asilimia 100 utoke katika walengwa husika. Ikiwa ni wanawake asilimia 100 ya uongozi ni lazima wawe wanawake.
Hata hivyo amesema katika kukamilisha utaratibu huo kwa taasisi hizo zitasajiliwa kwenye mfumo wa ununuzi na ndipo zitaanza kufanya maombi.