Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia walioshiriki Warsha ya Kitaifa ya siku mbili ya Wadau wa Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika jijini Dodoma leo. Waomsikiliza ni pamoja na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson (wa pili kulia) na Meneja Mpango wa CookFund wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Imanuel Muro (kulia). Hafla hiyo iliandaliwa na WFP na UNCDF kwa kushirikiana na wadau wengine.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akiwasikiliza wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia walioshiriki Warsha ya Kitaifa ya siku mbili ya Wadau wa Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika jijini humo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson (wa pili kulia) na Meneja Mpango wa CookFund wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Imanuel Muro (wa tatu kulia). Hafla hiyo iliandaliwa na WFP na UNCDF kwa kushirikiana na wadau wengine.
Meneja Mpango wa CookFund wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Imanuel Muro (kulia) akiwasilisha mada mbele ya wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia walioshiriki Warsha ya Kitaifa ya siku mbili ya Wadau wa Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika jijini Dodoma leo. Wanaomsikiliza ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) na Mkurugenzi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson (wa pili kulia) hafla hiyo iliandaliwa na WFP na UNCDF kwa kushirikiana na wadau wengine.
Mkurugenzi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson (kushoto) akiwasilisha mada mbele ya wadau mbalimbali wa nishati safi ya kupikia walioshiriki Warsha ya Kitaifa ya siku mbili ya Wadau wa Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika jijini Dodoma leo. Wanaomsikiliza ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) na Meneja Mpango wa CookFund wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Imanuel Muro (kulia) Hafla hiyo iliandaliwa na WFP na UNCDF kwa kushirikiana na wadau wengine.
Wadau wa sekta na nishati safi ya kupikia wajidali mada mbalimbali wakati wa warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki pamoja na waandaji wa warsha hiyo.
Hafla hiyo iliyohusisha wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Nishati, Chama cha Nishati Mbadala Tanzania (TAREA) na Chama cha Wadau wa Nishatio safi ya Kupikia Tanzania (TACCS), na Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira pia ilileta pamoja wajasiriamali wa teknolojia ya nishati safi ya kupikia , taasisi za utafiti, mashirika ya kijamii, mashirika ya Umoja wa Mataifa, taasisi za kifedha, mashirika ya ndani na kimataifa, taasisi za serikali na wadau wengine muhimu katika sekta ya nishati.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mtaji (UNCDF) kupitia Mpango wa CookFund unaofadhiliwa na EU kwa ushirikiano na wadau wengine wa sekta na nishati safi ya kupikia wamekutana mkoani Dodoma kwenye kongamano maalum kujadili ushiriki wao katika utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu kuhusiana dira na mkakati wa miaka 10 ya kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2033.
Kupitia kongamano hilo la siku mbili lililoratibwa na WFP na UNCDF , Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameibainisha kuwa tayari serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imeanza kuandaa muundo wa Mfuko maalum wa nishati safi ya kupikia nchini pamoja na dira na mkakati wa miaka 10 ya kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2033.
Akifungua kongamano la Kitaifa la Nishati safi ya kupikia, lililofanyika jijini Dar es Salaam Novemba mwaka jana, Rais Samia aliiomba wizara hiyo na wadau husika kuandaa mpango madhubuti utakaosaidia kuchochea mabadiliko ya asilimia 80 ya watu katika kupikia nishati safi ifikapo 2033.
“Wizara ya Nishati inaongoza maandalizi yote ya muundo wa mfuko huo kuelekea kufaniukisha adhmina hiyo ndani ya miaka 10 kulingana na agizo la Mheshimiwa Rais…niwafahamishe tu kwamba hadi kufikia sasa tunakwenda vizuri,’’ alisisitiza Mhandisi Mramba
Kwa mujibu wa Mhandisi Mramba tayari serikali imeunda timu maalum ya kitaifa ya nishati safi ya kupikia inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inahakikisha kwamba maagizo yote yaliyotolewa na Rais yanatekelezwa.
Hafla hiyo iliyohusisha wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Nishati, Chama cha Nishati Mbadala Tanzania (TAREA) na Chama cha Wadau wa Nishatio safi ya Kupikia Tanzania (TACCS), na Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira pia ilileta pamoja wajasiriamali wa teknolojia ya nishati safi ya kupikia , taasisi za utafiti, mashirika ya kijamii, mashirika ya Umoja wa Mataifa, taasisi za kifedha, mashirika ya ndani na kimataifa, taasisi za serikali na wadau wengine muhimu katika sekta ya nishati.
Akizungumza katika warsha hiyo Meneja Mpango wa CookFund wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Imanuel Muro, alisema kuwa shirika lake kupitia mpango huo unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) linaunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania akisisitiza:
“Tunazingatia juhudi za pamoja za kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2023 na ndiyo maana tumekuwa tukitoa ruzuku kwa sekta binafsi ili sekta hii iweze kuwasaidia watumiaji wa mwisho wa bidhaa hizo waweze kumudu gharama za vifaa vya nishati safi ya kupikia kwa kuwa vitapatikana kwa bei nafuu,” alisema. .
Katika hafla hiyo, Mkurugenzi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gordon-Gibson alisema: “Mwaka huu, WFP inapanga kusaidia karibu nusu milioni ya Watanzania wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wakimbizi wa Burundi na Kongo kupitia mipango mbalimbali. kwa kuwa watu wengi tunaowahudumia wanategemea kuni na mkaa kupikia.”
Kwa mujibu wa Sarah, upatikanaji wa nishati safi ya kupikia na teknolojia imekuwa ni changamoto kubwa na inayoleta athari mbaya za kiafya, jinsia, kiuchumi, mazingira na hali ya hewa.
Kwa hivyo, alibainisha, hatua za pamoja, zilizoratibiwa, na za kina na juhudi mpya zitahitajika ikiwa taifa linadhamilia kumaliza changamoto hiyo.
“Sera za kitaifa zinapaswa kuungwa mkono na uwekezaji wa umma na wa kibinafsi. Zaidi ya hayo, ushirikiano na mbinu mbalimbali za sekta mbalimbali na kazi nyingi zinahitajika ili kubadilisha namna tunavyopika nchini Tanzania, namna ambayo itaokoa maisha, kuboresha maisha, kulinda mazingira, na kuwawezesha wanawake na wasichana,” aliongeza.