Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akiwa katika kikao na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa (wa Tatu kulia) kilichofika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma. Wa Pili kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka. Wengine katika picha ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa (wa Pili kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumaliza kikao chao jijini Dodoma.Wengine katika picha ni watendaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (Wa Sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa (wa Tano kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka (wa Nne kushoto) mara baada ya kumaliza kikao chao jijini Dodoma. Wengine katika picha ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao chao jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amekutana na kufanya mazunguzo na Balozi Mpya wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa kuhusu kuendelea kushirikiana katika miradi mbalimbali ya Nishati nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika Machi 13, 2023 katika ofisi za Wizara ya Nishati Mkoani Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka pamoja na Viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Fedha na Ubalozi wa Japan nchini.
Katika mazungumzo hayo, Mramba ameishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati ukiwemo wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia.
Amesema, Tanzania ipo tayari kuendeleza ushirikiano na Japan katika kutekeleza miradi ya Nishati.
Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa alimueleza Katibu Mkuu huyo kuwa amekuja Wizara ya Nishati ili kujitambulisha na kueleza kuwa Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea ikiwepo ya kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia, kuzalisha umeme kutokana na Nishati Jadidifu hasa Upepo na ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Ameongeza kuwa, Japan imeendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali katika Sekta ya Elimu, Afya, Maji, pamoja Ujenzi wa miundombinu.
Baadhi ya miradi ya umeme ambayo inatekelezwa kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili ni pamoja na njia ya kusafirisha umeme ya msongo mkubwa wa Kilovolti 400 katika mradi wa Backbone na vituo vya Kupoza na Kusambaza Umeme katika maeneo mbalimbali nchini.