*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya yanga imefanikiwa kuiandibu Geita Gold Fc kwa mabao 3-1, katika mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam, nakuwafanya kufikisha pointi 65 baada ya kuingia uwanjani mara 24.
Katika mchezo huo tumeshuhudia Geita Gold Fc wakianza kupata bao dakika ya ya mchezo na kuwapeleka mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili Yanga Sc ilifanya mabadiliko ya wachezaji, wakitolewa Farid Mussa, Mudathiri Yahya pamoja na Djigui Diara huku wakiingia Mentacha Mnata, Jesus Moloko na Aziz Ki ambapo mabadiliko hayo yaliweza kuzaa matunda kwani walifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kenneth Musonda baada ya kupokea krosi kutoka kwa Lomalisa Mutambala.
Yanga Scc iliweza kufanikiwa kupata bao la pili la haraka kupitia kwa Clement Mzize baada ya Kenneth Musonda kupiga shuti kali na kipa kuokoa na kumkuta Mzize nakuzamisha nyavuni.
Bao la tatu la Yanga ambalo lilifunga mahesabu ya mabao kwenye mchezo huo limefungwa na winga machachali Jesus Moloko akipiga shuti kali lililomshinda kipa wa Geita Gold na kutinga nyavuni.