Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa zoezi la kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Mkurungezi Mtendaji wa Wilaya ya Kongwa Dkt Omary Nkullo,akizungumza wakati akitangaza mafanikio ya Halmashauri yake katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita.
Na Erick Mungele-DODOMA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katika miaka miwili ya Rais Samia inajivunia Mradi wa Ujenzi wa Kituo Mahiri cha Mafunzo kwa Wakulima na Usimamizi wa Mazao baada ya Mavuno katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati wa zoezi la kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa taasisi zilizopo Mkoani humo.
Mhe.Senyamule amesema kituo hicho pia Kitakuwa na utaalamu wa kuzuia sumu kuvu kwenye mazao na kitawezesha mazao kuuzika kimataifa na Mradi huu upo chini ya Wizara ya Kilimo na unagharimu takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 19 Ujenzi wake utakamilika Oktoba 2023.
“Wana Dodoma wana furaha sana na kuishukuru Serikali kwa utekelazaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo Mahiri cha Mafunzo kwa Wakulima na Usimamizi wa Mazao baada ya Mavuno Mtanana Kongwa lakini pia Kitakuwa na utaalamu wa kuzuia sumu kuvu kwenye mazao na kitawezesha mazao yetu kuuzika kimataifa. Mradi huu upo chini ya Wizara ya Kilimo na unagharimu takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 19,”amesema senyamule.
Aidha amesema wilaya ya kongwa wamenufaika na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa Kiwango cha lami barabara ya Arusha Kibaya Kongwa (km 430) kwa thamani ya Shilingi bilioni 2.5.
Kwa upande wake,Mkurungezi mtendaji wa Wilaya ya Kongwa Dkt Omary Nkullo amesema Vituo vya afya Vinavyotoa huduma vimeongezeka kutoka vituo 4 mwaka 2021 hadi vituo 8 mwaka 2022/2023. Aidha vituo 3 vituo 2 vimejengwa kwa fedha za TOZO na 1 Kinajengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri na utekelezaji wake umefikia hatua mbalimbali za ukamilishaji Ongezeko hili limesaidia Wananchi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.
Aidha amsema Jumla ya wastaafu 23 wamelipwa madeni yao yenye thamani ya Tshs.52,179,600 kwa kipindi cha 2021 hadi Februari, 2023. Aidha, watumishi wasio walimu 802 wamelipwa madeni ya malimbikizo ya mishahara yenye thamani ya Tshs Bilioni 1.01.
“Vituo vya afya Vinavyotoa huduma vimeongezeka kutoka vituo 4 mwaka 2021 hadi vituo 8 mwaka 2022/2023. Aidha vituo 3 vituo 2 vimejengwa kwa fedha za TOZO na 1 Kinajengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri na utekelezaji wake umefikia hatua mbalimbali za ukamilishaji. Ongezeko hili limesaidia Wananchi kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu,”amesema.
Hata hivyo, Miradi ya visima virefu, na maji ya mtiririko inayofanya kazi imeongezeka toka miradi 52 mwaka 2021 hadi 61 mwaka 2023 sawa na ongezeko la 17% na Idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama Vijijini umbali wa mita 400
imeongezeka kutoka 214,190 mwaka 2021 hadi 355,344 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la 65.9%.