Na Victor Masangu,Pwani
Wafanyakazi Wanawake wa shirika la ugavi wa umeme (Tanesco) Mkoa wa Pwani wametoa msaada wa mahitaji mbali mbali katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilaya ya Kibaha.
Wanawake hao wa Tanesco wameamua kufanya ziara katika kituo hicho kwa ajili ya kuwatembelea wanawake 40 ambao walikuwa wamejifungua katika wodi ya wazazi na kuwapatia msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo miche ya sabani,pampasi za watoto na mahitaji mengine.
Mwenyekiti wa wanawake hao wa Tanesco Selina Tarimo alisema kwamba wameamua kwenda kufanya matendo ya huruma katika wodi ya wazazi kwa lengo la kuweza kuwasalimia wakinamama ambao wamejifungua ikiwa pamoja na kuwapatia zawadi mbali mbali.
“Mimi pamoja na wafanyakazi wenzangu wa Tanesco tumeamua kuja katika kituo hiki cha afya mkoani lengo ikiwa ni kuwatembelea wakinamama 40 ambao wamejifungua na tumewapatia sabuni za unga.sabuni za miche,pampasi za watoto na mahitaji mengine muhimu,”alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema wao Kama wanawake wataendelea kushirikiana kwa umoja wao katika kuendelea kufanya matendo ya huruma pamoja na kuwasaidia wakinamama wengine ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali.
Nao baadhi ya wakinamama ambao wamepatiwa msaada huo wamewashukuru wafanyakazi Wanawake wa Tanesco kwa upendo wao wa kwenda kuwatembelea pamoja na kuwapatia msaada wa mahitaji yao tofauti.