Spika wa Bunge Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo Machi 11, 2023 ameongoza Kikao cha Kundi la SADC katika Umoja wa Mabunge Duniani (SADC Geopolitical Group in the IPU) kilichofanyika katika Ukumbi wa Paddock 6, Bahrain International Circuit (BIC), Manama, Bahrain kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)
Kulia ni Spika wa Bunge la Zimbabwe Mhe. Jacob Mudenda, kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Ndg. Yapoka Mungandi