********************
Na Lucas Raphael,Tabora
Katika hali isiyokuwa ya kawadia mwanaume mmoja amemuuwa mkewe na kuchimba shimo ndani ya chumba wanacholala na kumfukia humo na kulisakafikia kwa zege kutokana na madai ya wivu wa mapenzi .
Kauli hiyo ilitolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake jana ( Leo).
Alisema kwamba tukio hilo la mauaji liligundulika machi 7 mwaka huu majira ya saa 9.30 aliasiri katika mtaa wa mbilani kata ya Kidongo Chekundu Manispaa ya Tabora na mkoa wa Tabora na Michael Hendry baada ya kuona siku kadhaa zimepita bila chumba hicho kufunguliwa hivyo wakalazimika kuvunja mlango wa chumba cha kulala na kukuta chini ya kitanda kuna zege ilikiwa bado bichi alijakauka vizuri.
Alisema kwamba baada ya kuona hivyo alipata hofu iliyopelekea kufukua eneo hilo na kukuta mwili wa mtu umezikwa kwenye shimo hilo.
Kamanda Abwao alimtaja alifariki na kuzikwa ndani ya chumba chake cha kulala ni Salima Hamisi Maulidi (34) na chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Alisema kwamba mtuhumiwa baada ya kutekeleza unyama huo alimbia na jitiada za jeshi la polisi linaendelea kumsaka na kuwataka wananchi wema ambao wanafahamu muuaji alipo watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kumkamata na kisha kufikisha kwenye vyombo vya sheria ili kujibu mshitaka yanayomkabili .