Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia sehemu ya Maafisa Waandamizi, Bw. Mohamed Gombati wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bi. Felista Shuli akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Idara yake kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia sehemu ya Maafisa Waandamizi, Bw. Mohamed Gombati akitoa ufafanuzi wa majukumu ya sehemu anayoisimamia kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma.