WAZIRI wa Madini Dotto Biteko, akizungumza katika kikao cha kumtambulisha katibu mkuu Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini hafla iliyofanyika leo Machi 10,2023 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ,akizungumza wakati wa kikao cha kumtambulisha katibu mkuu Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini hafla iliyofanyika leo Machi 10,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba,akizungumza wakati wa kikao cha kumtambulisha katibu mkuu Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini hafla iliyofanyika leo Machi 10,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Watumishi wa wakimsikiliza Waziri wa Madini Dotto Biteko, (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kumtambulisha katibu mkuu Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini hafla iliyofanyika leo Machi 10,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Madini Dotto Biteko, akiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kikao cha kumtambulisha katibu mkuu Kheri Mahimbali, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini hafla iliyofanyika leo Machi 10,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Madini Dkt. Dotto Biteko, amemtaka katibu mkuu wa wizara hiyo aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan,kusimamia malengo na kuyafanyia kazi ili yakamilike kwa wakati.
Hayo ameyasema hayo leo Machi 10, 2023 jijini Dodoma kwenye kikao chake na watendaji wa Wizara na Tasisi zake wakati akimkaribisha na kumtambulisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali.
Dkt.Biteko amesema kuwa katika wizara hiyo wapo watu wa aina mbalimbali ambao katibu mkuu atakwenda kufanya nao kazi hivyo anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali kama ambavyo yamepangwa.
“Ndugu katibu mkuu hapa unaowaona wapo watu wa kila aina wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia ‘dead line’ hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamalizi kwa wakati na wala majibu hawakupi.
“lakini pia wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wanafurahi kurekebishwa lakini wengine ukiwarekebisha wanakukasilikia”amesema Biteko
Aidha, amesema kutokana na muda mwingi watumishi kuutumia wakiwa kazini katibu mkuu anatakiwa kuwafanya waajria kujiona wao ni wa muhimu katika wizara hiyo.
”Nakupongeza Katibu Mkuu mpya wa Wizara Mahimbali kwa uteuzi wako , Wizara na Taasisi zake itaendelea kukupa ushirikiano wa kutosha lengo likiwa ni kuifanya Sekta ya Madini kuwa miongozi mwa sekta zinazochochea uchumi wa nchi.”amesema Dk.Biteko
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa, amesema yapo mambo mengi ambayo wameyafanyia kazi hadi sasa ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamekaimu katika nafasi mbalimbali ndani ya wizara hiyo.
“Hivyo tunakuomba katika nafasi ambazo bado hazijafanyiwa kazi uone ni namna gani zinafanyiwa kazi ili maeneo yanayokaimiwa yapate watu na kazi ziendele kwa malengo tulijiwekea”amesema Dk. Kiruswa
Naye, Katibu Mkuu Mpya Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, amewataka wataalam wa Wizara kuweka msukumo kwenye madini ya Kimkakati kutokana na umuhimu wa madini hayo katika kuyafungamanisha na sekta nyingine za kiuchumi.
‘’Tumeletwa hapa kuongeza nguvu, sikuja kumwondoa yoyote kwenye nafasi yake, bado tuna kazi mbele yetu na ninaamini katika kushirikiana tutafika mmbalimbali katika kuyatimiza malengo ya Sekta ya Madini’’.amesema Mahimbali