Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido (kulia) na
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko (kushoto) wakiwalisha keki viongozi wa Wanawake katika mgodi huo wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, DK.Melkiory Ngido,akishiriki kukata keki wakati wa hafla ya wanawake wa mgodi huo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido, akiongea na Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa North Mara wakati wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick North Mara, wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dk.Melkiory Ngido( katikati) na Meneja Mkuu wa mgodi huo,Apolinary Lyambiko wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika mgodini hapo.
***
Meneja Mkuu wa Barrick Tanzania, Dk. Melkiory Ngido ,amewataka Wanawake kijiamini na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa madini.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye mgodi wa Barrick North Mara, Dk. Ngido alisema Barrick, inayo programu maalumu ya kuwapa wanawake kipaumbele katika suala la ajira , kuwajengea uwezo wa shughuli za uchimbaji madini na kuwajengea mazingira bora zaidi ya kazi.
“Msijisikie kuwa second class (daraja la pili), onesha kuwa mnaweza na naamini uwezo mnao,” alisema Ngido katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Wafanyakazi Wanawake kutoka mgodi huo.
Kwa upande wake,Meneja Mkuu wa mgodi huo,Bw.Apolinary Lyambiko, alisema anafurahishwa kuona idadi ya wafanyakazi wanawake katika mgodi huo imeongezeka uliganisha na miaka ya nyuma, na amewamiminia sifa kwamba wengi wao wanaonesha bidii na ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kazini.
“Takwimu za mwaka jana 2022 na sasa zinaonesha kuna ongezeko la wafanyakazi wanawake katika mgodi wetu, na wengi wao wanafanya kazi nzuri. Hivyo tutaendelea kuwapa fursa, siyo tu kujishughulisha na uchimbaji, bali na kuwamotisha pia,” amesisitiza Lyambiko na kuwataka kuendelea kuonesha uwezo mkubwa kazini na kujenga tabia ya kujiamini.
Lyambiko, alisema pia mgodi utaendelea kutekeleza sera yake ya kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakuwa katika kiwango cha sifuri katika mgodi huo.
Katika kuadhimisha siku hiyo wafanyakazi wanawake wa mgodi huo walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili mada mbalimbali za maendeleo sambamba na kupata burudani na kufurahi pamoja.