Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Profesa Edda Lwoga akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada kaika shule ya Sekondari ya Jangwani kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 ya kila mwaka.
Mfanyakazi wa CBE Asha mwenye ulemavu wa Kuona akizungumza katika Shule ya Sekondari Jangwani ikiwa ni kuwatia moyo wanafunzi wenye ulemavu na kwa kuwaambia ulemavu ni kipengele katika maumbile ambayo haizui kusoma.
Mfanyakazi wa CBE Dk.Mariam Tambwe mwenye ulemavu wa viunngo akizungumza katika Shule ya Sekondari Jangwani ikiwa ni kuwatia moyo wanafunzi wenye ulemavu na kwa kuwaambia ulemavu ni kipengele katika maumbile ambayo haizui kusoma ambapo kwake amefikia kiwango cha Udaktari. Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Profesa Edda Lwoga akikabidhi moja ya msaada ikiwa ni magongo ya kisasa mkuu wa shule sekondari Bhoke Nyaibuli kwa kushuhudiwa na mwanafunzi mwenye Ualbino Mratibu wa masuala ya Jinsia wa CBE Amanda Mollel akikabidhi msaa da vitu mbalimbali kwente Mahubusu ya Watoto Upanga.
Baadhi ya matukio mbalimbali ya Wafanyakazi wa CBE wakiwa katika majukumu ya utoaji msaada kwa wenye mahitaji maalum.
****************************
*Waahidi kwenda bega kwa bega kufikia ndoto zao
Na Mwandishi Wetu Wanawake wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wenye mahitaji maalumu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani na Watoto walioko katika Mahabusu ya Upanga Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa Kukabidhi msaada huo Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Edda Lwoga amesema kuwa msaada huo ni kutokana na kutambua watoto wenye wahitaji na wanawake ndio watu wa kwanza kutambua changamoto za watoto wenye mahitaji maalum.
Profesa Lwoga amesema wanawake wa CBE wameguswa kipekee na kujitoa kwa watoto wenye mahitaji na kuwatia moyo wanafunzi wa Jangwani kujituma katika kusoma kwani ulemavu haufanyi kushindwa kusoma.
Aidha amesema katika msaada waliotoa utasaidia kutatua baadhi ya changamoto kwani kama wanawake wametambua ni mahitaji gani yanatakiwa kwa watoto wenye mahitaji maalum.
Profesa Lwoga licha ya kutoa msaada wameweza kutoa msaada kwa Mfanyakazi mwenzao ambaye ana mtoto mwenye mahitaji maalum kwa kuamini hata wao wanahitaji kutambua baadhi ya wafanyakazi wenye changamoto ya watoto wao.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani Bhoke Nyaibuli ameshukuru msaada huo na kutaka baadhi ya Taasisi kuiga mfano mzuri kwa CBE.
Amesema katika Shule hiyo wanafunzi zaidi 900 huku wanafunzi 98 wakiwa na mahitaji maalum ambao, kila mmoja anakuwa na hitaji tofauti.
Mmoja Watumishi wa CBE Dkt. Mariam Tambwe amesema yeye ana ulemavu wa viungo lakini amesoma hadi kufikia Udaktari hivyo wanafunzi wenye ulemavu wasome kwa bidii kufika alipofikia au zaidi kwani ulemavu hauzuii kusoma.
Pia Bi. Asha Mfanyakazi wa ambaye nae ni mlemavu wa macho amewaasa wanafunzi wa Jangwani kujitahidi kusoma na kufikia malengo yao, kwani ulemavu hauwazuii kujiendeleza kufika viwango vya juu na kupata ajira.
Amewaasa Wasichana wenye ulemavu katika shule ya Jangwani wamshike elimu kuwa msaidizi wa pili wa kuwakwamua katika maisha yao ya sasa na baadaye.