Wanawake wa Wilaya ya Lushoto kwenye picha mbalimba walipokuwa wanagawa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Lushoto.
Na: Rosena Suka Lushoto
Katika kuhakikisha mtoto wa kike anawezeshwa kuhudhuria masomo na kupata elimu pasi na kufikiria changamoto ya kukosa taulo za kike awapo masomoni, na kumpunguzia changamoto hii kama si kuimaliza kabisa, leo Machi 7, 2023 kuelekeamaadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, wanawake wanaofanya kazi katika Taasisi za umma na binafasi Wilayani Lushoto wamekabidhi jumla yamaboksi 15 ya taulo za kike kwa MkurugenziMtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Mwasyoge.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri yaWilaya ya Lushoto, Bw. Eliza Moses wakati wakupokea msaada huo uliotoka kwa wanawake kutokaChuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, naTaasisi binafsi ya Usambara Development Instiativealiwashukuru sana kwa kuona umuhimu wakuwasaidia watoto wa kike walioko katika shule za msingi na sekondari wilayani humo. Bw. Eliezaaliendelea kwa kuziomba taasisi nyingine zijitokezekusaidia wanafunzi na kuelekeza kwamba ugawajiwa taulo kwa watoto wa kike iwe ni kampenimaalumu ya kunusuru na kuwakomboa watoto wakike.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii ambayeni Mratibu wa Maadhimisho ya siku wa wanawakeDuniani Bi. Fortunata Metusela akiongea kwa niabaya Mkuurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na wakatiwa ugawaji wa Taulo hizo kwa wanafunzi hao aliwaeleza kwamba wamepata msaada huo kwa ajiliya kuwastiri wakiwa katika siku za hedhi wanafunzi hao wasikose vipindi vya masomo wanapokuwa katika siku zao.
Bi. Metusela aliwasisitiza wanafunzi hao kuwaupatikanaji wa taulo za kike kwao ni msaadamkubwa ili kufanya vizuri kitaaluma kwa sababu hawatakosa vipindi vya masomo bali watahudhuria vyote, na kutoa wito kwa wanafunzi wafanye vizuri kitaaluma na kupata ufaulu mzuri. Aidha aliwawataka wanafunzi wa kike kujiepusha namazingira hatarishi ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia na endapo watakufanyiwa vitendo hivyo watoetaarifa kwa viongozi, wazazi au walezi wao Vilevile, amewataka pia wanafunzi wasome kwa bidii na kufaulu masomo yao, ambapo Serikali imeendelea kuwajengea miundo mbinu imara ya Shule, na mwaka huu Rais Samia ameshatoa tena fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari.
Shule ambazo zimefaidika na mgao wa taulo hizo za kike ni shule zilizoko katika pembezoni mwa wilaya ya Lushoto ambapo ni shule mbili za Sekondariambazo ni Prince Claude na Ubiri Sekondari ambapo Shule za msingi ni Bombo na Nyankei