NJOMBEWakazi wa vijiji vitatu vinavyounda kata ya Lupanga wilayani Ludewa mkoani Njombe wameiomba serikali kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa mradi wa kituo cha afya waliyoanza kuujenga tangu mwaka 2019 kwa kuchangishana fedha kwa zaidi ya miaka mine ,lengo likiwa ni kukoa maisha ya wagonjwa hususani watoto wachanga na wajawazito ambao wako hatarini kupoteza Maisha wakiwa njiani wakifata matibabu katika kituo cha afya cha Mlangali na Hospitali ya Wilaya ya Ludewa.
Kwa kuona ukubwa wa tatizo Hilo wakazi hawa wanasema walilazimika kuanza kuchangishana fedha kiasi cha elfu 10 kila mwaka ili kupata fedha za ujenzi wa mradi huo ambapo katika awamu ya kwanza walifanikiwa kujenga jengo la utawala na kisha baadae halmashauri ikahidi kuwashika mkono kwa kutoa mil 500 za ujenzi wa majengo mengine.
Wakieleza kuhusu changamoto za huduma za afya katika vijiji vyao nyenye wakazi zaidi ya elfu saba na jinsi inavyoathiri maisha ya watu wakazi hao akiwemo Faustino Joseph wanasema Kuna baadhi ya akina mama wajawazito walipoteza watoto wao wakiwa njiani kufata huduma, kwasababu ya umbali na ubovu wa barabara za kata hiyo iliyompakani mwa wilaya ya Ludewa na Makete.
“Tunaomba serikali itusaidie ujenzi wa kituo hiki Cha afya kwasababu walituahidi tukifanikishwa ujenzi wa Jengo la utawala watatusaidia fedha mil 500 za ujenzi wa majengo mengine ya kituo Cha afya,alisema Faistino Joseph mkazi wa Lupanga.”
Awali Silvanus Mlelwa ambaye ni katibu kata wa chama Cha Mapinduzi kata ya Lupanga amesema adha kubwa ya huduma za afya katika eneo hilo imekuwa ikiongeza chuki ya wananchi kwa chama hivyo wanaomba mbunge afanye kila linalowezekana kufanikisha ujenzi wa kituo Cha afya ili wagonjwa hususani akina mama wajawazito waepukane na tabu ya kusafiri umbali mrefu kufata matibabu kituo Cha afya Mlangali na Hospitali ya wilaya Ludewa
“Mh mbunge tunahofia kuchangisha Tena wananchi masuala ya maendeleo kwasababu Jengo hili limejengwa kwa nguvu za wananchi lakini tangu limejengwa hakuna kinachoendelea ,na nikuombe mbunge shughulikia hili la kituo Cha afya,alisema Silvanus Haule katibu wa CCM kata ya Lupanga”
Mbali na changamoto ya huduma za afya diwani wa kata ya Lupanga Dominicus Mganwa amemuomba mbunge kushughulikia Kero nyingine ya Barabara ili kufungua kata hiyo kiuchumi huku pia akisema endapo miundombinu ya Barabara itaimarika itasaidia pia kupunguza vifo visivyo vya lazima kwa wagonjwa.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Zakarius Kamonga akijibu hoja za wawakilishi wa wananchi kata ya Lupanga na maeneo mengine ya Jimbo Hilo anasema anaondoka na Kero ya kituo Cha afya na kuiwasilisha katika bunge la bajeti lijalo ili kiweze kutengewa fedha na serikali huku pia akisema hataishia bungeni bali atakwenda na halmashauri kufanya ushawishi kwa mkurugenzi.
Kuhusu Barabara Kamonga anasema imetengwa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa Barabara Bora inayotegemewa na kata ya Lupanga .
Katika mkutano huo mbunge huyo pia ametoa rai kwa wakazi wa Ludewa kuanza kujiandaa na machimbo ya mkaa wa mawe na chuma kwasababu serikali Iko kwenye hatua za mwisho za kuanza kulipa mfidia hivyo wakazi wote wa wilaya hiyo wawekeze katika majumba na vyakula kwakuwa soko lipo katika machimbo hayo.
“Nawaomba wote muanze maandalizi ya vitu vya kufanya ili tutakapopa fidia tusizichee,alisema mbunge wa Ludewa Joseph Kamong”