MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi 460 wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapingwa rushwa kutoka shule mbalimbali za Sekondari zilizopo Mkoani Dodoma.
MKUU wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo,akizungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi 460 wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapingwa rushwa kutoka shule mbalimbali za Sekondari zilizopo Mkoani Dodoma.
MKUU wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,,akizungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi 460 wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapingwa rushwa kutoka shule mbalimbali za Sekondari zilizopo Mkoani Dodoma.
SEHEMU ya wanafunzi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi 460 wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapingwa rushwa kutoka shule mbalimbali za Sekondari zilizopo Mkoani Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamuleakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi 460 wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapingwa rushwa kutoka shule mbalimbali za Sekondari zilizopo Mkoani Dodoma.
Na.Erick Mungele-DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kulifanyia kazi suala la uanachama wa kudumu kwa wanafunzi wanaohitimu,ili kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa rushwa, ikiwemo kutambulika hata kama watakuwa wamemaliza masomo yao.
Senyamule ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi 460 wa kidato cha sita ambao ni wanachama wa klabu za wapingwa rushwa kutoka shule mbalimbali za sekondari zilizopo mkoani Dodoma.
Amesema kuwa elimu walioipata shuleni kuhusu nidhamu na uadilifu kwenye suala zima la rushwa wanapaswa kuiendeleza wakiwa uraiani,hususani utoaji elimu kwa raia ambao hawana uelewa na madhara ya kutoa na kupokea rushwa.
”TAKUKURU inapaswa kulifanyia kazi,ili wanapomaliza waweze kutambulika na kuendelea kutoa elimu ya kupiga vita rushwa kwa jamii.”amesema RC Senyamule
Hata hivyo Senyamule amezipongeza klabu za wapinga rushwa ambazo ziko hai,huku akisisitiza kuendelea kuzisimamia kwa sababu zinawajenga vijana tokea awali kukataa rushwa ambayo inachangia kupata viongozi wazembe.
Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo ,amesema jukumu la kupiga vita rushwa ni la kila mmoja,hivyo wanafunzi wanaohitimu nao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwenye kupiga vita rushwa kutokana na elimu walioipata katika klabu za kupinga rushwa.
“Vijana hawa wameiva vizuri katika masuala ya rushwa,naamini wanakwenda kuwa mabalozi wazuri wakiwa uraiani,”amesema Bw. Kibwengo.
Naye ,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,amesema katika shindano la mdahalo kuhusu kupiga vita rushwa,baina ya shule na shule amepanga kutoa zawadi nzuri kwa shule ambayo itafanya vizuri katika shindano hilo,tofauti na shindano lililopita.