Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali mara baada ya kufungua kongamano hilo jijini Arusha
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela amesema kuwa, agenda ya kumwinua mwanamke wa Afrika katika masuala ya biashara inatekelezwa kwa vitendo,huku serikali ikiahidi utoaji wa mikopo .
Ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa kongamano la 2 linaloangalia biashara kwa wanawake ujulikanao kama African business women & youth (Tawen) unaofanyika jijini Arusha kwa siku 3.
Mongela amepongeza mafanikio makubwa ya wanawake katika ubunifu na uwajibikaji ,na kueleza serikali ya Samia imeendelea kuhakikisha agenda ya kumwinua mwanamke inafikiwa katika nyanja zote.
“Serikali imeendelea kusisitiza kutengwa kwa fedha za mikopo ya asilimia 10 ndani ya halmashauri Ili kusaidia wanawake vijana na makundi maalumu kuwezesha kufanyabishara.”amesema .
Florence Masunga ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika hilo la (Tawen) amesema kuwa, dhamira kubwa ya kufanyika kongamano hilo jijini hapa ikiwemo kuyafikia masoko na kuwepo kwa soko huru la biashara ndani na nje ya nchi.
Aidha wadau mbalimbali walichangia mada huku wakiwataka vijana kuhakikisha wanachangangamkia fursa mbalimbali za ajira ikiwemo kujiajiri kwa kutafuta biashara ya kufanya ambayo ni ya tofauti na hizi zilizopo sokoni hivi sasa.
“Vijana lazima wafike mahali wajiajiri wao wenyewe na wafanye biashara ambazo ni za tofauti ili waweze kupata masoko mengi zaidi badala ya kukaa tu bila kuwa na shughuli yoyote ya kufanya kwani fursa zilizopo ni nyingi sana.”amesema.
Aidha vijana hao wakizungumza katika kongamano hilo waliomba wadau mbalimbali pamoja na serikali kuwaunga mkono katika shughuli zao wanazofanya kwani changamoto kubwa imekuwa ni ukosefu wa masoko ili kufikia malengo yao.