NA K-VIS BLOG
Mbunge wa jimbo la Mbagala, jijini Dar es Salaam, Mhe. Abdallah
Chaurembo ameahidi kutoa TZS Milioni 2 kukamilisha ujenzi wa Kituo Kidogo Cha
Polisi (Police Post), Kata ya Mbagala-Kiburugwa.
Ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
viwanja vya Njau, Kata ya Kiburugwa Machi 4, 2023.
Alisema Kituo hicho kimejengwa kutokana na michango ya
wananchi, Mbunge na Diwani wa Kata hiyo.
“Nadhani mmeona maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa Kituo
chetu Cha Polisi, kazi iliyobaki ni kupaua, mimi kama Mbunge wenu nitatoa shilingi
Milioni 2,000,000/= ili tukamilishe ujenzi kwa kuezeka.”Alisema.
Kuhusu msongamano wa wanafunzi, Mhe. Chaurembo amesema Shule
ya Msingi Kingugi yamejengwa madarasa mawili (2) na Shule ya Msingi Kiburugwa yamejengwa
madarasa mapya 2 na vyoo 18 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 59.8.
Kiburugwa yamejengwa madarasa 2 yenye thamani a shilingi Milioni
40,
Jumla ya Fedha zilizotumila kuboresha zaidi ya shilingi
Milioni 100.
Aidha alisema mgogoro uliokuwepo wa nyumba za makazi zilizokuwa
ndani ya eneo la shule ya Sekondari Kingugi umetatuliwa kwa wamiliki wake kulipwa
fidia na nyumba hizo kubomolewa na kujengwa
madarasa 4.
“Madarasa hayo yamekamilika na wanafunzi wanaingia madarsani.”
Alifafanua.
Kuhusu miundombinu ya barabara, alisema kwa muda mrefu imekuwa
ndio kilio kikubwa cha wananchi wa Kata ya Mbagala Kiburugwa.
“niliwaahidi moja ya kipaumbele changu ni barabara ya kutoka
Kona Bar, Magenge 20, tayari awamu ya kwanza imeanza ya ujenzi, na sasa tunaanza
awamu ya pili na bilashaka mmeona wakandarasi wako kazini.” Alisema na kuongeza..
Jumla ya shilingi Milioni 391 zimetumika
kuboresha barabara za Kiburugwa kwa kiwango Cha Zege”. Alifafanua Mhe.
Chaurembo