Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
ABIRIA waliokuwemo katika bus la Happy Nation lililokuwa likitokea Kagera -kwenda Dar es Salaam wamenusurika kifo ,baada ya bus Hilo kupinduka upande wa kushoto eneo la Vigwaza , Mkoani Pwani.
Katika ajali hiyo wapo majeruhi sita waliofikishwa hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi kwa matibabu zaidi.
Akithibitisha juu ya kutokea kwa ajali hiyo , wakati alipofika hospital ya Tumbi kuangalia hali ya majeruhi hao, Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa ,alhaj Abubakari Kunenge Alisema ,ajali hiyo imeelezwa Kuwa imetokea majira ya saa 8:30 usiku Machi 2 mwaka huu.
Alieleza , majeruhi walikuwa idadi kubwa lakini walipatiwa huduma kwanza Kituo Cha afya Mlandizi na wengine waliruhisiwa ,na sita wapelekwa hospital ya Tumbi kwa matibabu zaidi.
“Tumefika hospital ya Tumbi ,eneo la emergency room, tumethibitisha hospital yetu imepokea majeruhi sita hadi sasa waliotokana na ajali hiyo,
“Idadi ya majeruhi ilikuwa kubwa ambapo walikimbizwa kituo Cha afya Cha Mlandizi na kupatiwa huduma ,kisha wengine waliruhisiwa kuendelea na shughuli zao nyingine “
Kunenge alitoa rai kwa madereva, kuzingatia sheria za usalama barabarani,kwani dereva wa bus anadaiwa kufanya uzembe wa kutaka kulipita roli upande wa kushoto na kusababisha bus kulalia upande huo.
“Madereva waepuke kufanya uzembe ,ambao unaweza kusababisha madhara makubwa , Tunashukuru hakuna kifo kwenye ajali hii,Lakini majeruhi wapo ,wanasababishiwa majeraha ya viungo ambapo kama dereva angefuata sheria yasingetokea haya”alifafanua Kunenge.
Nae mganga mfawidhi hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi, Amani Malima alieleza ,ni kweli wamepokea majeruhi sita wa ajali hiyo na kuambiwa wengine watatu wapo njiani kupelekwa hospitalini hapo.
Alisema Kuwa ,majeruhi hao wameumia zaidi maeneo ya mkono,mabega, mgongo lakini wanafanyiwa vipimo vya x-ray na CT-scan ili kupatiwa matibabu endapo watakuwa na madhara yatakayoonekana kitabibu.
“Majeruhi Hawa wa awali wote wameshaanza kupatiwa matibabu,na wanaendelea vizuri, licha ya kwamba watafanyiwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi “alieleza Malima.
Jeshi la polisi mkoani Pwani limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na, taarifa zaidi juu tukio hilo zitaendelea kutolewa.