NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM  

KATIKA kuhakikisha wanaunga mkono suala la usafi wa Mazingira, Kampuni ya Betika imeandaa mashindano ya SODO 4 CLIMATE ambayo yanafanyika katika fukwe za Coco Beach Jijini Dar es Salaam.

Mashindano ya sodo ni mchezo wa mpira wa miguu ambao mpira ambao wanauchezea ni mpira ambao umefumwa kwa kutumia  kamba maalumu ambayo  mara nyingi huchezwa wachezaji wakiwa hawana viatu.

Akizungumza na  Mwandishi wetu Jijini Dar es Salaam leo Machi 1,2023, Afisa Habari wa Betika, Juvenalius Rugambwa amesema katika Mashindano  hayo  timu ya Friends  of Tulia Trust ambayo nayo imepata fursa ya kushiriki  imeweza kuenguliwa baada ya kupokea kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa timu ya Espanyol.

Amesema lengo la mashindano hayo nikuhamasisha jamii katika suala la usafi ambapo wameweza  kufanya usafi katika  fukwe za bahari na kutoa elimu ya hamasa kwa jamii kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.