MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele,akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari pamoja na Waandishi wa Habari leo Machi 1,2023 (hawapo pichani) kuelekea Maadhimisho ya wiki ya JKT yatafanyika kuanzia Julai mosi, na kilele kuwa Julai 10 Mwaka huu ambayo yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii, michezo mbalimbali na maonyesho ya kazi zinazofanywa na SUMA JKT na JKT jijini Dodoma.
MKUU wa Tawi la utawala wa JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza kuelekea Maadhimisho ya wiki ya JKT yatafanyika kuanzia Julai mosi, na kilele kuwa Julai 10 Mwaka huu ambayo yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii, michezo mbalimbali na maonyesho ya kazi zinazofanywa na SUMA JKT na JKT jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo Kanali George Kazaula,akielezea Maadhimisho ya wiki ya JKT yatafanyika kuanzia Julai mosi, na kilele kuwa Julai 10 Mwaka huu ambayo yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii, michezo mbalimbali na maonyesho ya kazi zinazofanywa na SUMA JKT na JKT jijini Dodoma.
SEHEMU ya Wahariri wa Vyombo vya habari na Wadau wa Maadhimisho hayo wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele (hayupo pichani) wakati,akizungumza kuelekea Maadhimisho ya wiki ya JKT yatafanyika kuanzia Julai mosi, na kilele kuwa Julai 10 Mwaka huu ambayo yataambatana na shughuli mbalimbali za kijamii, michezo mbalimbali na maonyesho ya kazi zinazofanywa na SUMA JKT na JKT jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-CHAMWINO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye Amir Jeshi Mkuu Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa JKT Julai 10 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 1,2023 Jijini Dodoma Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele amesema maadhimisho ya miaka 60 ya JKT yanayotarajiwa kufanyika katika maeneo mbalimbali na kilele kufanyika Julai 10 katika uwanja wa Jamhuri Jijini.
Meja Jenerali Mabele amesema kuwa kuelekea siku ya kilele kutakuwa na wiki ya JKT ambayo itaanza Julai Mosi mwaka huu hadi Julai 9 mwaka huu ikiambatana na shughuli ikiwemo mashindano ya mbio za riadha (JKT MARATHON) ambayo itafanyika jijini Dodoma Juni 25 mwaka huu kwa lengo la Kujenga Afya za watanzania.
”Kutakuwa na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali ,mashindano ya bonanza kwenye michezo mbalimbali ambayo itafanyika viwanja vya Chinangali Park na Chuo Kikuu Cha Dodoma pamoja na maonesho ya vikundi vya Sanaa na utamaduni kutoka katika vikundi vilivyopo ndani ya JKT ambayo shughuli ambazo zitafanyika katika maeneo ya Nyerere Squre na SUMA JKT House.”amesema Meja Jenerali Mabele.
Aidha amesema JKT itashirikiana kikamilifu kupitia vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kuhusiana na namna JKT linavyoendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni malezi ya vijana,uzalishaji Mali na ulinzi,sanjari na namna JKT lilivyojipanga kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika kuadhimisha miaka 60 tangu kuasisiwa kwake Julai 01 ,1963.
Hata hivyo Meja Jenerali Mabele amesema kupitia fedha zinazotolewa na serikali wanazitumia katika kuboresha makambi ya Jeshi ili kuhakikisha JKT linachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha sita kwenda kupata mafunzo ya uzalendo na ukakamavu.
Meja Jenerali Mabele amesema SUMA JKT ,kwa nyakati tofauti limeanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji Mali na huduma kupitia Sekta za ujenzi ,uhandisi na ushauri,sekta ya Kilimo,mifugo na Uvuvi ,sekta ya viwanda pamoja na sekta ya huduma na biashara lengo likiwa kujiongezea kipato.
“Hii imesaidia kupunguza mzigo wa kibajeti kwa Serikali wa uendeshaji wa shughuli za JKT ,miundombinu ya Makambi ya zamani Serikali imekuwa ikiyaboresha pamoja na kuanzisha Makambi mapya bila kuathiri majukumu ya msingi.”amesema Meja Jenerali Mabele.
Aidha Meja Jenerali Mabele amesema JKT kupitia kilimo mkakati ambapo hivi sasa Jeshi linajitosheleza kwa baadhi ya mazao kama vile mahindi na mchele unaotokana na uzalishaji katika vikosi mbalimbali hapa nchini na kwamba lengo ni kihakikisha ifikapo 2024/25 Jeshi hilo liweze kujitegemea kwa chakula.
Maadhimisho hayo yataongozwa na Kauli mbiu isemayo”Malezi ya vijana,uzalishaji Mali na ulinzi kwa ustawi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la utawala wa JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema JKT mbali na shughuli nyingine linatimiza majukumu yake ya msingi ya malezi kwa vijana na kuwafundisha stadi za maisha.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo Kanali George Kazaula amesema maandalizi yanakwenda vizuri na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo yatakayoambatana na shughuli mbalimbali za Kijmaii.