Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akizungumza wakati
wa maafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Coastal High School ya
Jijini Tanga yaliyofanyika kwenye Hotel ya CBA Jijini Tanga
Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti
mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal
High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya shule hiyo,Lulu George
Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti
mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal
High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya shule hiyo,Lulu George
Na Oscar Assenga,Tanga.
Shule
ya Sekondari Coastal ya jijini Tanga,itaanza kunufaika na uwekezaji wa
sekta ya mkonge baada ya Bodi ya Mkonge Tanzani (TSB) kuahidi kuiingiza
katika majaribio ya klabu za vijana watakaoendelezwa.
Pia shule hiyo imeahidiwa kupewa ekari 100 kwa ajili ya kilimo cha mkonge ikiwa ni sehemu ya kuiongezea kipato .
Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Mko n ge nchini,Saad Kambona alitoa ahadi hiyo wakati
wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita walioanza mtihani ya
kitaifa.
Alisema bodi hiyo imeandaa programu maalumu
itakayowawezesha vijana kujiinua kiuchumi kuptia kilimo cha mkonge na
bidhaa zitoakanazo na zao hilo.
Alisema kama inavyofahamika Bodi
ya Mkonge ni taasisi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ni kama imekufa sasa
imeshafungua rasmi ofisi katika jengo lake na kuwezesha kuinua sekta
ya mkonge kwa ujumla wake.
“Lakini tunategemea tunapokwenda
mbele vijana wengi sana kutoka kwenye shule za Tanga ndiyo wahusike
kwenye mpango mzima wa kuleta mapinduzi kwenye zao la mkonge kwani sasa
hivi tunapozungumzia mkonge tunazungumzia bidhaa moja tu ya nyuzi za
mkonge zitengeneze vikapu, makapeti, magunia, kamba na bidhaa nyingine
zitokanazo na zao hilo ,lakini kuna bidhaa nyingti zinahitajika kama
sukari,mbolea mvinyo na hata vyakula vya kunenepesha mifugo” alisema
Kambona
Mkuu wa shule hiyo,Joseph Gaspar alisema ilianza rasmi
mwaka 2000 na kwamba kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikitoa ufaulu
wa daraja la kwanza A na pili kwa wanafunzi wote wa kidato cha sita
wote katik a mitihani ya kitaifa ya mchepuo wa sayansi.
“Hadi
sasa shule hii imetimiza miaka 22 lakini kwa kipindi cha miaka miatatu
mfululizo i mekuwa ikitoa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza na
la pili katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha sita…tunatarajia
mitihani hii ufaulu utakuwa wajuu zaidi”alisema Gasper.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George alisema kwamba
kuwa miongoni mwa mambo yanayotiliwa mkazo ni masomo ya sayansi
wakiamini kuwa jukumu lao ni kupata wataalamu watakaoiendeleza nchi
katika sekta ya uhandisi,udaktari na utafiti mbalimbali ikiwamo sekta
ya kilimo na ufugaji.