Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti ya Wizara baada ya kupokelewa katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma. Tukio Februari 27, 2023.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka (wa kwanza kushoto) akikabidhiwa ua na mmoja kati ya Maafisa wa Wizara ya Nishati Bi.Talkisia Eriyo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mji wa Serikali Mtumba. Tukio Februari 27, 2023.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka (wa tatu kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato (wa kwanza kulia), mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati. Tukio Februari 27, 2023
Wengine katika Picha ni Watumishi wa Wizara ya Nishati wakimpokea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka wakati alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Tukio Februari 27, 2023.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba (wa kwanza kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Menejimenti wa Wizara ya Nishati mara baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Athuman Selemani Mbuttuka kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Februari 27, 2023
Na Dorina G. Makaya – Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ameomba kupatiwa ushirikiano mzuri kutoka kwa uongozi na watumishi wa Wizara ya Nishati ili kumwezesha kutekeleza vyema majukumu yake.
Athumani Selemani Mbuttuka aliyasema hayo jana alipokutana na Menejimenti ya Wizara ya Nishati baada ya kuripoti ofisini kwake Wizara ya Nishati kufuatia kuteuliwa na kuapishwa kwake tarehe 27/02/2023 kuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Alisema atajitahidi kutekeleza majukumu yake ipasavyo na anaamini kuwa uzoefu katika uongozi alionao Katibu Mkuu Mha. Felchesmi Mramba utasaidia katika kumjenga zaidi katika kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Mramba, alisema Wizara ya Nishati imepata mtu muhimu mwenye uzoefu katika mifumo ya Serikali wakati alipokuwa akisimamia mashirika yote ya Serikali kama Msajili wa Hazina na wakati akiwa Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu za Serikali na anaamini uzoefu wake utasaidia katika kuboresha utendaji hususan kwenye eneo la utawala bora.
Katibu Mkuu Mramba aliahidi kumpatia ushirikiano mzuri Naibu Katibu Mkuu Mbuttuka na kuishukuru Menejimenti ya Wizara ya Nishati na watumishi kwa kumpatia mapokezi mazuri na kuwataka wampatie ushirikiano mzuri Naibu Katibu Mkuu huyo ili kumwezesha kutekeleza majukumu yake vyema.
Naibu Katibu Mkuu Mbuttuka alishukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata Wizara ya Nishati na kuahidi kushirikiana vema na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara ya Nishati katika kuendeleza Sekta ya Nishati nchini.