MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 28,2023 jijini katika Mwendelezo wa Programu maalumu ya kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA.
Mkurugezi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 28,2023 jijini katika Mwendelezo wa Programu maalumu ya kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ndani ya kipindi cha miaka miwili katika Mamlaka hiyo.
Na Eric Mungele-DODOMA
KATIKA kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita madarakani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,Mkoa wa Dodoma unajivunia ongezeko la upatikanaji wa maji kutoka wastani wa lita Milioni 61.5 mwaka 2020/2021 hadi kufikia 67.8 Milioni mwaka 2022/2023.
Hatua hiyo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana yanaoenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambayo imeahidi kufikisha kiwango cha maji kwa mijini kwa asilimia 95 na vijijini asilimia 85.
Hayo yameleezwa leo Februari 28,2023 Jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati wa kuwasilisha taarifa ya mafanikio ya serikali kwa kipindi cha miaka miwili upande wa sekta ya maji.
RC Senyamule amesema Uzalishaji umeongezeka kutoka Lita Mil. 61.5 na kufika 67.1 kwa siku, Chamwino Upatikanaji wa maji Umeongezeka kutoka 42% mpaka 87%,Kongwa Upatikanaji wa maji Umeongezeka kutoka 44% hadi 88%,Bahi Upatikanaji wa maji Umeongezeka kutoka 37% hadi 95%.
Pia amesema Katika kukabiliana na ongezeko kubwa la mahitaji ya Maji jijini Dodoma, Serikali kupitia Wizara ya Maji na DUWASA imewekeza kiasi cha Tsh. 9.14bilioni ambapo Uchimbaji na uendelezaji wa visima (32) sehemu mbalimbali za huduma, ufungaji wa pumpu, ulazaji wa kilometa 208.86 za mtandao wa kusafirishia na kusambazia maji, ujenzi wa Matenki yenye ujazo wa lita 3,035,000.
“Uzalishaji umeongezeka kutoka Lita Mil. 61.5 na kufika 67.1 kwa siku, Chamwino Upatikanaji wa maji Umeongezeka kutoka 42% mpaka 87%,Kongwa Upatikanaji wa maji Umeongezeka kutoka 44% hadi 88%,Bahi Upatikanaji wa maji Umeongezeka kutoka 37% hadi 95%. na takwimu hizi zinafanya kuvuka malengo ya chama cha mapinduzi.
“Katika kukabiliana na ongezeko kubwa la mahitaji ya Maji jijini Dodoma, Serikali kupitia Wizara ya Maji na DUWASA imewekeza kiasi cha Tsh. 9.14bilioni ambapo Uchimbaji na uendelezaji wa visima (32) sehemu mbalimbali za huduma, ufungaji wa pumpu, ulazaji wa kilometa 208.86 za mtandao wa kusafirishia na kusambazia maji, ujenzi wa Matenki yenye ujazo wa lita 3,035,000,”amesema Senyamule.
Kwa upande wake,Mkurugezi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph ameelezea mafaniko yaliopatika na matarajio kwenye taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili.
Mhandisi Joseph ameelezea kuwa Mkoa wa Dodoma unahudumia wakazi 765,179 kwa mujibu wa (Sensa.2022) ambapo takribani 91% wanapata huduma ya Majisafi na salama (Kwa Mgao) na 20% huduma ya uondoshaji Majitaka hata hivyo Mahitaji ya Maji ya Jiji la Dodoma kwa sasa ni lita 133,400,000 kwa siku, na yataongezeka hadi lita 417,308,000 kwa siku hadi kufikia Mwaka 2051.
Aidha ameelezea Uwezo wa vyanzo vyote vya maji vya DUWASA ni lita 67,100,00 kwa siku na Upungufu wa mahitaji ya maji ni lita 66,300,000 kwa siku sawa (50%) Mahitaji ya mfumo wa kutibu Majitaka ni lita 20,000,000 kwa siku Uwezo wa mfumo wa kutibu Majitaka ni lita 350,000 kwa siku na Upungufu wa uwezo wa kutibu Majitaka ni lita 19,650,000 kwa siku.
“kwa sasa Jiji la Doodoma ina wakazi 765,179 nahii ni mujibu wa (Sensa.2022) ambapo takribani 91% wanapata huduma ya Majisafi na salama (Kwa Mgao) na 20% huduma ya uondoshaji Majitaka hata hivyo Mahitaji ya Maji ya Jiji la Dodoma kwa sasa ni lita 133,400,000 kwa siku, na yataongezeka hadi lita 417,308,000 kwa siku hadi kufikia Mwaka 2051.
“Uwezo wa vyanzo vyote vya maji vya DUWASA ni lita 67,100,00 kwa siku na Upungufu wa mahitaji ya maji ni lita 66,300,000 kwa siku sawa (50%) Mahitaji ya mfumo wa kutibu Majitaka ni lita 20,000,000 kwa siku Uwezo wa mfumo wa kutibu Majitaka ni lita 350,000 kwa siku na Upungufu wa uwezo wa kutibu Majitaka ni lita 19,650,000 kwa siku,”amesema
Hata hivyo ameelezea,Katika kukabiliana na ongezeko kubwa la mahitaji ya Maji jijini Dodoma, Serikali kupitia Wizara ya Maji na DUWASA imewekeza kiasi cha Tsh. 9.14bilioni kwa hatua za muda mfupi za kupunguza uhaba wa maji ambayo ni Uchimbaji na uendelezaji wa visima (32) sehemu mbalimbali za huduma, ufungaji wapumpu, ulazaji wa kilometa 208.86 za mtandao wa kusafirishia na kusambazia maji, ujenzi wa Matenki yenye ujazo wa lita 3,035,000.
Pia Bwawa la Farkwa Tayari Serikali imetenga Dola 125.3 million kwa ajili ya kujenga Bwawa na Mtambo wa Kutibu Maji kupitia AfDB Mradi huu utaongeza kiasi cha Maji lita Milioni 128 kwa Siku. Mradi upo katika hatua za kuwapata wahandisi washauri wa mradi ukiunganisha lakini Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria amabao Upembuzi wa awali ulifanyika na kukamilika mwezi Desemba, 2019 umeonesha uwezekano mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria kufika Dodoma na Mradi huu unalenga kuhudumia Mji wa Dodoma na Singida.
“katika mapngo wa muda mrefu na mfupi Bwawa la Farkwa Tayari Serikali imetenga Dola 125.3 million kwa ajili ya kujenga Bwawa na Mtambo wa Kutibu Maji kupitia AfDB Mradi huu utaongeza kiasi cha Maji lita Milioni 128 kwa Siku. Mradi upo katika hatua za kuwapata wahandisi washauri wa mradi ukiunganisha,”amesema Joseph.
Aidha ameeleza changamoto zinazo ikabili DUWASA nihubaribifu wa miondombinu ya maji safi na taka kuharibiwa na wanachi wanaozunguka na kuowaomba wauza vyuma chakavu kuacha kununua vifaa vya mali ya serikali licha ya kununua vyuma chakavu wanasaidia kutunza mazingira.