Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
SHULE ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere (MJNLS) imeonyesha matunda baada ya kuwanoa viongozi wa vyama rafiki waliopata mafunzo uongozi ya muda mfupi takriban 189 na waliotoka kwenye Taasisi mbalimbali 728 huku walioshiriki midahalo wakiwa 1,700.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Wajumbe wa Chama Cha CPC ambao uliongozwa na Naibu Waziri wa Mahusiano ya Nje Li Mingxiang kukagua maendeleo ya shule, mkuu wa shule hiyo Profesa Marcelina Chijoriga ameeleza, wanaendelea kutoa mafunzo mbalimbali.
Chijoriga amesema ,mafanikio waliyoyapata ni baadhi ya viongozi wa vyama hivyo waliopata mafunzo wameweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwemo Dk Batilda Buriani mkuu wa mkoa wa Tabora na wanayapima mafunzo kwa kiongozi kwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi.
Chijoriga amesema ,nchi ya China walikuwa kama sisi miaka ya 60 iliyopita lakini wamepiga hatua kwa viongozi kuketa mabadiliko,ushirikiano ,uzoefu ,ukuaji wa kimaendeleo na ujenzi wa uongozi kwa shule kama ya (China National Academy of Governance) ambapo wao wana shule zaidi ya 2,000.
Vilevile,ameeeza katika uendeshaji kuna changamoto ya fedha ,hawapati ruzuku hivyo wanachokifanya ni kuongea na Taasisi mbalimbali ili wawapatie mafunzo na kufanya midahalo, mikutano na kuchangiwa na vyama rafiki.