KLABU ya Yanga imelazimishwa sare na timu ya Real Bamako kwenye hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika baada ya Kutoka sare ya Magoli 1-1 Dhidi ya Real Bamako ya Mali.
Katika mchezo huo, Yanga haikuweza kucheza mpira mzuri kipindi cha kwanza kwani hawakutengeneza nafasi kwenye lango la upinzani mpaka mapumziko ambako timu zilienda zikiwa hazijapata bao.
Kipindi cha pili timu zote ziliingia zikihitaji bao kwani ziliweza kutengeneza nyingi licha ya Yanga kutumia vizuri nafasi moja na kuweza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Fiston Kalala Mayele ambaye alipokea pasi kutoka kwa Aziz Ki.
Real Bamako katika dakika za lala salama waliweza kupata bao la kusawazisha kupitia kona ambayo ilizaa bao.
Yanga Sc sasa itakuwa inashika nafasi ya tatu kwenye kundi lao wakiwa wamecheza mechi tatu na kujikusanyia pointi nne ikiwa anaeongoza Monastir akiwa na pointi saba.