Afisa Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania, Mike Ndaisaba akiongea na wageni waliyetembelea Banda la Wizara ya Maliasili na utalii katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.
Mdau wa utalii aliyetumia tukio la Kilimanjaro Marathon kupeperusha bendera ya Tanzania na kutangaza utalii kwa kuvaa vazi lenye picha ya mnyama anayepatikana nchini Tanzania.
Washiriki wa Kilimanjaro Marathon wakipata picha ya kumbukumbu ndani ya banda la wizara ya Maliasili na Utalii.
******************************
Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki katika mashindao ya Klimanjaro Marathon. Bodi na taasisi hizo zimetumia mashindano haya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania, majukumu yanayotekelezwa na kila Taasisi pamoja na fursa nyingine za uwekezaji zilizopo katika sekta ya Utalii Tanzania.
Mashindano haya ya Kilimanjaro Marathon yanafanyika kila mwaka yamezidi kupata umaarufu na yamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza utalii wa michezo nchini Tanzania, ambapo yameweza kuwavutia watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani kushiriki katika mashindano haya.
Mashindano ya mwaka huu yameanza na matukio tofauti ya maonesho ya bidhaa mbalimbali za mazao ya utalii yaliyoanza tarehe 24, 25 na 26 Februari, 2023 katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika kilichopo Mkoa wa Kilimanjaro na yanahitimishwa leo kwa washiriki kukimbia mbio zilizogawanywa katika makundi matatu; Mbio ndefu za Kilometa 21, Mbio za Kati Kilometa 21 na mbio fupi za Kilometa 5.
Taasisi zilizoshiriki katika banda la Wizara ya Maliasili na utalii ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Malaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), Mamlakaya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS).