JUMUIYA ya Wazazi cha cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar ea Salaam wameunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo ili kuweza kuhakikisha Jumuiya ya Wazazi ya mkoa huo inakuwa dira ya mkoa na inayokwenda kusimamiwa ndani ya miaka mitano kuweza kuhakikisha inatekeleza 2022/2023 kusimamia mipango kazi ambayo wamejiwekea kwa miaka mitano.
Akizungumza katika sherehe za kuwakabidhi barua za uteuzi wanakamati leo Februri 25,2023 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa Dar ea Salaam Bi.Khadija Ally Said amesema anategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwenye kamati zilizoundwa katikakuhakikisha kazi za jumuiya ya wazazi ndani ya mkoa wa Dar es salaam wanazitendea haki,
Kamati ambazo zimeundwa na kutangazwa ni kamati tano ambazo ni Kamati ya Miradi, Uchumi na Maendeleo, Kamati ya Utamduni, Michezo na Mazingira, Kamati ya Elimu, Afya na Malezi,Kamati ya Nidhamu na Maadili pamoja na Kamati ya Habari za Jumuiya.
Akizungumza kuhusu Kamati ya Elimu, Afya na Malezi Bi.Khadija amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi, malezi ni ajenda yeao kitaifa, ndo maana wanakuja na kauli mbiu ya “Malezi bora kwa Mtoto , Faraja ya Kesho ya Mzazi na Taifa”, ambapo kamati hii inawataalamu ambao wataenda kufanya mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya kata, pia kamati hii ina viongozi wa kiroho.
“Kamati hii inaenda kusimamia mambo ya msingi sana ya malezi na maadili lakini pia suala zima la elimu kuhakikisha ufaulu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa watoto wa shule za Msingi na Sekondari unakua, lakini tunaenda kuanzisha shule za awali ambayo kupitia hii kamati wataweza kutuanzishia umuhimu wa shule za awali katika ngazi ya kata, wilaya lakini kuhakikisha kwamba jumuiya ya wazazi inasimamia elimu katika ubora wake na afya vilevile”. Amesema
Aidha amesemaKamati ya miradi, Uchumi na Maendeleo inaenda kusaidia kwa kiwango kikubwa ndani ya Mkoa kwani katika sera za siasa na uchumi lazima tuwe na miradi ambayo iko katika hali sahihi na watafanya kazi katika miradi ambayo Jumuiya ya Wazazi itaweza kubuni, kusimamia na kuiongoza kuhakikisha wanabadilisha hali ya wanajumuiya wake katika ngazi ya kata, Wilaya na Mkoa lakini pia kufanya miradi ambayo inapeleka jumuiya na chama cha mapinduzi moja kwa moja na wananchi katika kuongeza kipato chao.
Pamoja na hayo, miongoni mwa Kamati ambazo zimeundwa, kuhusu Kamati ya Utamduni, Michezo na Mazingira, amesema kuwa katika kujenga mahusiano yetu lazima tuingie kwenye michezo, kwahiyo watakuwa na timu za wazazi katika kata zao, watakuwa na mashindano ya michezo mbalimbali katika kata, wilaya na katika ngazi ya mkoa.
“Tunategemea kama tukifanya vizuri kuingia na kwenda hata nje ya nchi kupitia timu zetu , na hii ni kwaajili ya kupanua wigo wa mahusiano kati ya Chama lakini pia na wananchi wake kwahiyo michezo ndio sehemu peke yake watu wanakutana kwa pamoja”. Amesema .
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya ya Elimu, Afya na Malezi Bw.Ismail Sadick (Suma lee) amesema atajitahidi kushirikiana na wajumbe wengine kuhakikisha suala la elimu na malezi linakuwa bora katika Mkoa wa Dar es Salaam kwasababu katika Kamati hiyo wapo viongozi wa kiimani ambao pia wataenda kushirikiana nao.